TAARIFA
KWA UMMA
MAADHIMISHO YA
SIKU YA ARDHIOEVU DUNIANI TAREHE 2 FEBRUARI 2018
Tanzania pamoja
na nchi wanachama wa Mkataba wa Uhifadhi
Ardhioevu (Ramsar Convention) inafanya maadhimisho ya siku ya ardhioevu duniani
Fe kila mwaka. Ardhioevu ni maeneo yenye ardhi chepechepe yaliyopo kandokando
na ndani ya Chemchemi, Mito, Maziwa na mwambao wa bahari wenye kina cha mita
sita wakati wa kupwa. Ardhioevu pia hujumuisha Madimbwi, Mabwawa, Matingatinga
na sehemu zote yanapokusanyika maji kipindi kirefu cha mwaka. Asilimia 10 ya
ardhi ya Tanzania ni Ardioevu. Nchini kuna ardhioevu yenye umuhimu wa Kimataifa
yajulikanayo kama Maeneo ya Ramsar. Maeneo
ya Ramsar nchini yapo manne ambayo ni; Ziwa Natron yenye umuhimu wa kuhifadhi
ndege aina ya Heroe Wadogo- (Lesser flamingo), Malagarasi Muyovosi ina umuhimu wa kuhifadhi ndegemaji aina
ya Korongo Domokiatu (Shoebill Stork),
Bonde la Mto Kilombero yenye umuhimu wa uhifadhi wa Puku na Rufiji mafia Kilwa
uhifadhi wa Mikoko na Mazao ya Baharini.
Ujumbe wa mwaka
huu ni: "Ardhioevu kwa Maendeleo Endelevu ya Miji”. Ardhioevu ni sekta
endeshi ya uchumi wa nchi kwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika kwenye nyumbani,
kilimo, uzalishaji wa umeme na uhifadhi wa wanyamapori ambao ni kivutio cha
utalii nchini. Ardhioevu huzuia majanga ya mafuriko, hupunguza athari za kiafya
zinazoweza kujitokeza kutokana na madini hatarishi kama Zebaki.
Hata hivyo, ardhioevu
nchini zinaharibika na zingine kutoweka kutokana na
ongezeko la shughuli za kimaendeleo zisizo endelevu kama vile ujenzi kwenye
vyanzo vya maji, ufugaji holela, kilimo kisichozingatia kanuni za kilimo cha
kisasa na kukata miti ovyo. Athari zingine ni pamoja na vifo vya mimea maji na
wanyama wanaotegemea maji kuishi na kunywa kutokana na matumizi yasiyoendelevu
kama viboko, samaki na mamba.
Mamlaka inatoa
wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya Ardhioevu kushirikiana na Serikali
kuyatunza maeneo haya kwa kutekeleza sheria mbalimbali za uhifadhi ikiwemo Sheria
ya Uhifadhi Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009, Sheria ya Mazingira ya mwaka
2004 na Sheria zingine za kisekta kama ya Maji na Uvuvi na kuwahimiza wale wote
wanaoishi kwenye maeneo ya ardhioevu na hifadhi kuhama sawa.
Imetolewa na,
MKURUGENZI
MKUU
2 February 2018
0 comments:
Post a Comment