BARAZA LA WAFANYAKAZI FCC JUKWAA MUHIMU LA KUIMARISHA MSHIKAMANO NA UTENDAJI KAZI KWA WATUMISHI
Baraza la wafanyakazi Siri ya utendaji bora
Na Mwandishi Wetu
BARAZA la Wafanyakazi la Sita la TMDA limefanyika kwa ufanisi tarehe 5-6 Februari, 2026 katika Manispaa ya Morogoro, kwa kuwakutanisha wajumbe wa Menejimenti na kutoka kwa Watumishi wa TMDA kwa lengo la kujadili na kukubaliana masuala mbalimbali ya kitaasisi yenye mchango mkubwa katika kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka.
Miongoni mwa ajenda kuu zilizojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kutoa maoni na mapendekezo kuhusu Mpango Mkakati wa TMDA wa miaka mitano (2026/27 – 2030/31), Rasimu ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27, pamoja na Mpango wa Mazingira, Jamii na Utawala (Environmental, Social and Governance – ESG).

Akifunga kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TMDA ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Dkt. Adam Fimbo, aliwashukuru wajumbe wa Baraza kwa maoni yao ambayo yalilenga kujenga na yanayolenga kuboresha utendaji kazi wa taasisi, akisisitiza kuwa wafanyakazi ni sehemu muhimu ya TMDA na mchango wao ni nguzo ya mafanikio ya Mamlaka.
“Baraza la Wafanyakazi ni jukwaa muhimu la ushirikishwaji na uwazi katika maamuzi ya taasisi. Mawazo na maoni yenu yamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mifumo ya utendaji na kulinda afya ya jamii,” alisema Dkt. Fimbo.

Baraza la Wafanyakazi la TMDA linajumuisha wawakilishi kutoka Menejimenti na Watumishi, na hukutana mara mbili kwa mwaka kwa mujibu wa sheria na miongozo ya utumishi wa umma.
Lengo kuu la mikutano hiyo ni kujadili taarifa za utendaji kazi wa TMDA, kubaini fursa na changamoto zilizopo, pamoja na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha mifumo na huduma za Mamlaka.

Kupitia Baraza la Wafanyakazi, TMDA imekuwa ikiimarisha mshikamano, uwajibikaji na mawasiliano ya wazi kati ya Menejimenti na Watumishi, hali inayosaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa zingine zinazodhibitiwa, kwa lengo la kulinda afya ya jamii.

TMDA itaendelea kuthamini mchango wa Baraza la Wafanyakazi kama chombo muhimu cha ushirikishwaji katika maamuzi ya kimkakati na uendeshaji wa taasisi, sambamba na azma ya kujenga mazingira bora ya kazi na kutoa huduma bora kwa jamii.
TPHPA yaahidi kufuatilia changamoto ya Nzi weupe Nyandira Wilayani Mvomero zilizotolewa na wakulima kupitia mradi AGRISPARK - SUA
Na: Calvin Gwabara – Mvomero.
Kufuatia taarifa za athari kubwa za Nzi Weupe kwenye mazao ya
mbogambona Wilayani Mvomero zilizoibuliwa na wakulima
wakati wa utekelezaji wa mradi wa AGRISPARK Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu Tanzania
(TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru ameahidi kutuma timu ya
wataalamu kwenye wilaya hiyo kuona athari na kufanya oparesheni
ya kuwatokomeza wadudu hao.
![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya afya ya mimea na viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Ndunguru (Picha kwa msaada https://afrikaleo.co.tz/) |
RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN APONGEZA NSSF NA JESHI LA MAGEREZA KUKAMILISHA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI
RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN APONGEZA NSSF NA JESHI LA MAGEREZA KUKAMILISHA MRADI WA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI
*Asema mradi huu una umuhimu wa kipekee
*Asema kiwanda hicho kinaenda kutoa uhakika wa sukari nchini, awapongeza NSSF na Jeshi la Magereza kwa kufanikisha mradi huo
Na MWANDISHI WETU,
MOROGORO. Historia imeandikwa na hakika hakuna kilichokwama! Unaweza kusema hivyo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua rasmi mradi wa kiwanda cha sukari Mkulazi, kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro na kusema mradi huo anataka uwe endelevu kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Uzinduzi wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka umefanyika tarehe 7 Agosti, 2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali. NSSF kupitia mradi huo imetekeleza moja ya jukumu lake la uwekezaji; majukumu mengine ni kuandikisha wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo, kukusanya michango na kulipa mafao.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla hiyo Mhe. Rais Dkt. Samia amewapongeza wana hisa wa kiwanda hicho ambao ni NSSF na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SHIMA), kwa kukamilisha mradi huo wenye manufaa makubwa na kuwa Serikali inafanya kila jitihada kutanua mradi huo.
Aidha, amepongeza mradi huo kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania pamoja na wakulima kupata soko la uhakika wa kuuza miwa. Pamoja na hilo amepongeza mradi huo kutumia umeme ambao unaozalishwa kiwandani hapo. Amesema dhamira na malengo ya Serikali ni kuhakikisha mradi huo unakua na kuleta tija kubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ujenzi wa kiwanda hicho unatokana na maono ya Rais Dkt. Samia ambaye aliahidi kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ukiwemo wa Mkulazi. Amesema baada ya Rais Dkt. Samia kuingia madarakani mwezi Machi 2021, aliridhia mradi huo kuendelea na kuwa unaenda kupunguza nakisi ya sukari nchini na kutatua changamoto ya ajira.
Amesema uwekezaji wa mradi huo umeongeza wigo wa kodi na umechechemua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa ziara yake katika mkoa huo ambayo imekuwa na mafanikio makubwa hasa katika kuzindua miradi ya kimkakati ukiwemo wa kiwanda cha sukari Mkulazi ambao umetoa fursa nyingi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akitoa taarifa ya mradi wa kiwanda hicho, Dkt. Hildelitha Msita, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mkulazi, amesema wataendelea kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuondoa nakisi ya sukari nchini pamoja na kuongeza ajira kwa Watanzania kwa kusimamia uendeshaji wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 50,000 za sukari kwa mwaka na tayari uzalishaji wa sukari ya majumbani ulianza tarehe 1 Julai, 2024 ambapo kwa siku kinazalisha tani 250.
Kwa upande wake Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amesema mradi huo umekuwa na faida kwa Jeshi la Magereza na kuwa faida hizo zinatokana na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia kuhakikisha wanatumia vizuri rasilimali za Jeshi hilo kwa kuleta tija na kutoa mchango kwa jamii na Taifa.
Naye Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema uwepo wa mradi wa kiwanda hicho unatoa fursa mbalimbali kwa wananchi, hivyo watahakikisha kiwanda hicho kinazalisha sukari ya majumbani na viwandani na kinalindwa kwa maslahi mapana ya Taifa.
Aidha, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara, amesema Serikali ya awamu ya sita imeweka historia kubwa ikiwemo kuongeza idadi ya viwanda takribani 18,000 ndani ya miaka mitatu.
Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Profesa Kalamagamba Kabudi amesema wananchi wa jimbo hilo wanashukuru ujio wa kiwanda hicho ambacho kinawasaidia kupata ajira na kupata soko la uhakika la kuuza miwa yao.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua Daraja la Berega, Kilosa Mkoani Morogoro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi Daraja la Berega lililopo Wilayani Kilosa katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi Mkoani Morogoro tarehe 02 Agosti, 2024.
Warsha ya Kitaifa Kujadili Shabaha za Kuondoa Uharibifu wa Ardhi na Mbinu Shirikishi ya Tathmini ya Ardhi (ILAM) Yafanyika Morogoro
Wataalamu na wadau wa sekta mbalimbali nchini walishiriki katika warsha ya siku mbili kwa ajili ya wajumbe wa Kitaifa wa Shabaha za Kuondoa Uharibifu wa Ardhi (Land Degradation Neutrality National Working Group – LDN WG) sambamba na mafunzo ya Mbinu Shirikishi za Tathmini ya Ardhi (Integrated Land Assessment Methodology – ILAM).
Akifungua warsha hiyo iliyoandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Miombo ya Nyanda Kame Tanzania jijini Morogoro, Dkt. Deogratius Paulo, Mkurugenzi Msaidizi-Ofisi ya Makamu wa Rais, aliwataka wataalamu na wadau hao kuhakikisha kuwa warsha hiyo inakuwa chachu ya kufanikisha shughuli za utekelezaji wa mradi sambamba na juhudi za kitaifa na kimataifa za kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.
“Ninafahamu kwamba warsha hii imewakutanisha pamoja wataalam kutoka wizara za kisekta, taasisi za serikali, mamlaka za serikali za mitaa, washiriki wa maendeleo, asasi zisizo za kiserikali na sekta binafsi. Nyinyi ni miongoni mwa wataalam wachache ambao tunatarajia kuwa mabalozi wa kufuatilia shabaha za kupambana na uharibifu wa ardhi katika sekta zenu, huku mkiangalia mbinu za usimamizi shirikishi za kuondoa uharibifu wa ardhi.
Ni dhahiri kuwa tusipofanya kazi kwa ushirikiano kama ambavyo tumeitwa hapa, tutashindwa kufanikiwa. Hivyo, niwaite nyie kuwa 'you’re the champions of LDN na ILAM,' mabalozi wa utekelezaji wa shabaha za kupambana na uharibifu wa ardhi na hivyo kunusuru nchi yetu na ukame na jangwa,” alisema Dkt. Paulo.
Awali, Mratibu wa Mradi na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi – TFS, Zainabu Shabani Bungwa, akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Prof. Dos Santos Silayo, alitoa shukrani kwa Shirika la FAO na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano wao katika kutekeleza mradi huu, ambao unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira ya Dunia (GEF).
“Lengo kuu la mradi ni kukomesha na kubadili mwelekeo mbaya wa uharibifu wa ardhi na upotevu wa bioanuwai katika maeneo yaliyoharibiwa ya misitu ya miombo kusini-magharibi mwa Tanzania. Utatekelezwa katika maeneo ya Tabora (Kaliua Landscape) katika Wilaya za Kaliua, Urambo na Sikonge; Katavi (Mlele Landscape) kwa thamani ya dola za Marekani milioni 6.875, sawa na shilingi bilioni 16.8, kwa kipindi cha miaka mitano (2022-2027),” alisema Kamishna Msaidizi huyo.
Aliongeza kuwa moja ya shughuli za mradi huo ni kujenga uwezo wa wataalam na sekta mbalimbali katika masuala ya usimamizi shirikishi ili kuhakikisha huduma za kiokolojia kutoka katika Misitu ya Miombo zainaimarika. Alisisitiza kuwa mradi huu tutapiwa kwa uzalishaji bora wa asali na mnyororo wa thamani wa mazao ya nyuki na mengine ya kilimo.
Aidha, watalam watawezeshwa pia tathmini ya rasilimali za misitu, na manunuzi ya baadhi ya vitendea kazi katika maeneo yao. Huku akizitaja shughuli nyingine kuwa ni urejeshwaji wa ardhi iliyoathiriwa, mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi, ujenzi wa vituo vya ulinzi wa misitu (ranger posts), Vituo vya kukusanya na kuchakata asali, nyumba za kufugia nyuki (bee cages) na kuwezesha upatikanaji wa vyanzo vya maji na vituo vya utunzaji wa mbegu za miti na kilimo.
Kwa kumalizia, Kamishna Msaidizi Bungwa aliwashukuru wote waliowezesha kikao hicho na kuhimiza kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha uhifadhi wa misitu, ufugaji wa nyuki, na utalii.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na wajumbe wapatao 40.

























.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)














.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)