Ujenzi wa korido ya Kituo cha Afya Mtimbira ukiendelea.
Moja ya jengo lililojengwa katika Kituo cha AfyaMtimbira likiwa katika hatua za mwisho za umaliziaji.
Moja ya jengo lililojengwa katika Kituo cha AfyaMtimbira likiwa katika hatua za mwisho za umaliziaji.
Mwonekano wa baadhi ya wodi zilizofanyiwa ukarabati katika Kituo cha Afya Mtimbira.
Na. Mwandishi wetu Malinyi
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Marceline Ndimbwa amempongeza Mganga
Mkuu wa Kituo cha Afya Mtimbira kwa kusimamia vizuri ujenzi na ukarabati
wa Kituo cha Afya Mtimbira.
Aliyasema
hayo wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati na ujenzi unaoendelea
katika Kituo hicho cha Afya lengo likiwa ni kujiridhisha na kazi
zinazofanyika katika kituo hicho.
Akiongea
kituoni hapo Ndimbwa alisema kazi nzuri imefanyika kutokana na
mwonekano wa baadhi ya majengo yaliyokamilika ambayo yanaendana na fedha
iliyotolewa lakini pia usimamizi mzuri wa Mganga Mkuu wa kituo na timu
yake.
Aliongeza
kuwa serikali imetoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa Kituo hicho hivyo
ni jukumu la wananchi na viongozi wote kusimamia ujenzi huo na
kuhakikisha kuwa unakamilika kwa wakati ili wananchi wapate huduma bora
za Afya.
Aidha
alisema kuwa fedha zilizotolewa ni kwa ajili ya ukarabati wa majengo
yote ya zamani ambayo yameshakamilika kukarabatiwa na ujenzi wa majengo
mapya sita katika kituo hicho unaendelea ikiwemo jengo la upasuaji, wodi
ya kinamama, chumba cha kuhifadhia maiti, maabara, wodi ya wanaume na
kujenga kichomeataka.
Hata
hivyo wananchi kwa pamoja walijitolea nguvu zao kwa kuchangia kiasi cha
shilingi milioni kumi na saba ikiwa ni kuunga mkono jitihada
zilizofanywa na serikali kwa kuwaboreshea huduma za Afya.
Kituo
cha Afya Mtimbira ni moja ya vituo vilivyopata fedha kutoka Serikalini
ambapo jumla ya shilingi milioni mia tano zimetolewa kwa ajili ya
kuboresha kituo hicho kwa kukarabati majengo ya zamani na kujenga
majengo mapya.
0 comments:
Post a Comment