Kikosi Kazi kinachojumuisha
Sekta kuu za matumizi ya Ardhi na Asasi za Kiraia wamekutana kwa ajili
kuendelea kurejea Mwongozo wa ushirikishaji katika kupanga mipango ya matumizi
ya Ardhi pamoja na kukamilisha kazi ya rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na
changamoto zinazoikabili mipango ya matumizi ya ardhi ikiwemo kuutafsiri kwa
lugha ya kiswahili.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume
ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Dkt. Stephen Nindi, pamoja na
kupongeza kazi nzuri ambayo inafanywa na kikosi kazi, lakini pia lizungumzia
swala la mipango miji,upangaji wa mipango bora ya matumizi ya ardhi
utakaozingatia mtazamo wa kuipeleka nchi katika Dira ya viwanda na pamoja na
swala la mabadiliko ya Tabianchi, ili wananchi wawe tayari kukabiliana na
changamoto ya mabadiliko ya Tabianchi kunatakiwa kuwe na mipango mizuri ya
matumizi ya ardhi.
Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu,
Sera na Mawasiliano wa TumeBi. Albina Burra akitoa maelezo mafupi kwa
Mkurugenzi wa Tume hiyo Dkt. Stephen Nindi kuhusiana na kazi kazi ya kikosi
kazi ya kukamilisha andiko la Mkakati wa changamoto za mato za matumizi ya
Ardhi ikiwa ni pamoja na kuandaa mwongozo na kubadili andiko kwa lugha ya
kingeleza ili lipate kusomwa na wafadhiri pia wadau wengine.
Afisa Mipango kutoka Tume ya
Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald Mwakipesile (wa kwanza kulia)
akiwapitisha kikozi kazi katika maeneo mbalimbali ya kukamilisha mkakati wa
kutatua changamoto za matumizi ya Ardhi nchini.
Afisa Tawala wa Tume ya Taifa
ya Mipango ya matumizi ya Ardhi Bi. Nakivona Rajabu akitoa mrejesho wa kikao
kilichofanyika na Mh. William Lukuvi Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi alipokuwa anakabidhiwa Rasimu ya Mkakati wa kukabiliana na changamoto za
matumizi ya Ardhi cha tarehe 14.08.2017 mjini Morogoro.
Wanakikosi kazi wakiwa wanafuatilia mrejesho huo
Wanakikosi kazi wakiwa katika
makundi kwa ajili ya kushirikiana kwa pamoja kulibadili andiko la mkakati wa
kukabiliana na changamoto za matumizi ya Ardhi kwa lugha ya kingeleza ili uweze
kuja kusomwa na wafadhiri pamoja na wadau wengine mbalimbali.
Bw. Emmanuel Msofe kutoka
Wizara ya Maliasili na Utalii, akitoa maoni yake wakati wa mkutano huo.
Bwana Daniel Ouma(kushoto)
Afisa Miradi kutoka TNRF akichangia jambo wakati kikosi kazi kikiendelea na
kazi.
Bw. Mbaraka Stambuli kiongozi
wa Kipengele cha maendeleo ya kisera na kitaasisi katika programu ya kuwezesha
umilikishwaji wa Ardhi, akichangia jambo la maboresho wakati wa kubadilisha
andiko katika lugha ya kingeleza.
Bwana Herman Nyanda Afisa
wanyama pori (TAWA) mwandamizi katika dawati la ushirikishwaji jamii katika
uhifadhi wa wanyama pori akichangia hoja wakati shughuli ya kubadilisha andiko
katika lugha ya kingeleza inaendela
Kikosi kazi wakiendelea na kazi
Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa
0 comments:
Post a Comment