Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini mkoani Morogoro ,Semina hiyo imeratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)
Mwezeshaji wa semina Joe Nakajumo akifundisha katika mafunzo hayo leo Mkoani Morogoro
Kushoto ni Noria Damian ,katikati Editha Carlo pamoja Happines Mtweve wakifatilia mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uandishi wa habari za vijijini wakifatilia mafunzo hayo kwa ukaribu
Amon Mtega kutoka Ruvuma Press club akiachangia mada katika mafunzo hayo ,kulia ni Queen Isack kutoka Kilimanjaro Press Club
Kushoto ni mwakilishi kutoka Arusha Press club Pamela Mollel,katikati ni Adam Juma kutoka Mtwara Press Club wakifatilia mafunzo
Mwandishi wa habari Laudence Simkonda kutoka Mbeya kulia Oscar Simon kutoka Rukwa wakifatilia mafunzo hayo
Na Pamela Mollel,Morogoro
Waandishi
hapa nchini wametakiwa kuongeza muamko katika kuandika na kutangaza habari za
vijijini kwa kuwa asilimia 75ya wananchi wa Tanzania wanaishi vijijini ambako
wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli mbalimbali
Rai hiyo
ilitolewa leo Mkoani Morogoro na mwenzeshaji Joe Nakajumo katika mafunzo ya uandishi wa
habari za vijijini iliyowakutanisha wanahabari kutoka mikoa mbalimbali
iliyoratibiwa na umoja wa vilabu vya habari Tanazania(UTPC)
Nakajumo
alisema kuwa waandishi wa habari wanajukumu kubwa la kuwa karibu na jamii ya
vijijini kwa kutambua shughuli zao wanazozifanya na kuzifatilia kwa kuona
mafanikio yao pamoja na kuibua kero zinazowakabili
“Asilimia 75
ya wananchi wanaishi vijijini wanaendesha maisha yao kwa kufanya shughuli za
kilimo,ufugaji ,uvuvi,ujasiriamali hivyo ni muhimu sana kuwapa kipaumbela
wananchi hawa”alisema Nakajumo
Aidha
alisema kuwa moja ya majukumu ya msingi ya mwandishi wa habari ni kusaidia na
kushiriki katika ujenzi wa taifa hivyo anapaswa kuudhihirishia umma kwa watu
wote nchini wanapaswa kupata habari
Kwa upande
wake mshiriki wa semina hiyo Adam Juma alisema kuwa mafunzo haya yatasaidia
kuibua changamoto vijijini ambako panaoneka kusaulika kwa huduma mbalimbali za
kijamii
Pia
aliwaomba waandaji wa semina hii UTPC kuendeleza mafunzo haya kwa waandishi wa
habari ili kuweza kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya
taaluma hiyo
Umoja wa
vilabu vya habari Tanazania(UTPC)imekuwa ikiendelea kutoa mafunzo mbalimbali
kwa waandishi wa habari lengo ikiwa kuwaongezea ujuzi wa kufanya kazi zao kwa
kufata misingi ya taaluma .
0 comments:
Post a Comment