Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akiwa na Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Masijala ya Kijiji Cha Nyange ambayo itakuwa inatunza kumbukumbu ya hati.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi ,akizungumza na Wakazi wa Kijiji Cha Nyange Kabla ya kuanza zoezi la Ugawaji hati za Kimila kwa wakzi wa Kijiji Hicho ambao wamepimiwa kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Wiliam Lukuvi akimkabidhi hati yake Mkazi wa Kijiji Cha Nyange , Bibi Clesencia Namuhoni wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
Balozi wa Denmark nchini ,Einar Hebogard akizungumza na wakazi wa kijijii cha nyange juu ya umuhimu wa kumiliki hati za kimila katika kujiendeleza kiuchumi wakati wa hafla ya kukabidhi hati za kimila katika kijiji hicho kupitia mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
Mratibu wa Programu, Godfrey Machabe mpango wa kuwezesha umilikishaji wa Ardhi (Land Tenure Support Programme) uliofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia Uk Aid,Serikali ya Sweden SIDA na Denimark kupitia DANIDA.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii , Kilombero
Waziri
wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wananchi kuacha
kuuza maeneo yenye hati za kimila na kuwaonya kuwa maeneo hayo yamepimwa
na serikali zaidi hawatatozwa kodi kwa wananchi wanaomiliki ardhi za
kimila na maofisa arddhi wawatoze kodi wale wenye hati za miaka 99 za
umiliki wa mashamba makubwa ya biashara.
Lukuvi
ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa hatimiliki za kimila
zaidi ya 2000 katika Kijiji cha Nyange wilayani Kilombero mkoa wa
Morogoro kupitia Mradi wa Uwezeshaji Umilikishaji Ardhi (LTSP).
Lukuvi
amesema hatimiliki hizo zipo kwa lengo la kulinda ardhi ya vijiji
husika na kwamba walanguzi wa ardhi hawatapata nafasi kwa kuwa ardhi
iliyopimwa haitaweza kununulika kwa mtu ambaye sio wa kijiji hicho.
Amesema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya udalali wa ardhi
lakini kutokana na ulinzi uliowekwa katika hatimiliki hizo, hawataweza
kwa kuwa ardhi haitanunulika.
"Hili
ni agizo kutoka kwa Rais Dk John Magufuli kwamba wananchi wote
watakaopatiwa hatimiliki za kimila wasitozwe kodi isipokuwa wale wenye
mashamba makubwa ya biashara ambao watatozwa kila ekari Sh 1,000. Kwa
kuwa hamtalipa kodi, basi fedha hiyo muitumie kuzalisha zaidi kwa
manufaa yenu ya baadae," alisema Lukuvi na kuongeza;
"Ardhi
iliyopangwa na kupimwa hata kama ardhi ni ndogo inathamani kubwa zaidi
ya mtu mwenye eneo kubwa ambalo halina hatimiliki."
Alisisitiza
kuwa wananchi waliopewa hatimiliki za kimila wanakopesheka hivyo, benki
zote zifungue milango na kuwapatia mikopo stahiki ili kuendeleza
mashamba yao na kujiinua kiuchumi. Alieleza kuwa maofisa wa serikali
wanapaswa kueleza namna ya kuzalisha mazao mengi kuliko awali na kwamba
ardhi isibadilishwe matumizi kama ni ya kilimo au ufugaji itumike kama
ilivyotakiwa.
Lukuvi
amesema katika miaka ijayo wanatarajia kutoa hati za kimila 300,000 kwa
wananchi na kwamba kwa sasa asilimia 20 pekee ya ardhi ndio imepimwa na
kupangwa.
LTSP
ni mradi wa majaribio wa miaka mitatu unaofadhiliwa na Mashirika ya
maendeleo ya Denmark kupitia Shirika la DANIDA na nchini Sweden kupitia
Shirika la SIDA na Uingereza kupitia Shirika la UKaid ambapo kwa sasa
ni katika Wilaya za Kilombero, Malinyi na Ulanga mkoani Morogoro. Mradi
huo umeanza Julai mwaka jana kwa kazi ya kupima, kubainisha mpango wa
matumizi ya ardhi.
0 comments:
Post a Comment