WAKULIMA nchini wameshauriwa kutumia mbegu ya mahindi ya WEMA ambayo
inastahimili ukame hasa kwenye maeneo yote yanayopata mvua kidogo.
Mtafiti wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga wilayani Kilosa
mkoani Morogoro, alisema jana kuwa mbegu hiyo mpya inastawi kwenye
udongo wenye unyevu kidogo mahindi yanastawi na kutoa mazao mengi. Mbegu
hiyo imefanyiwa utafiti na watafiti wa Tanzania kuanzia mwaka 2008 na
tayari kwa sasa imeshaingizwa kwenye soko la Tanzania tayari kutumiwa na
wakulima.
“Lengo la kuleta mbegu hii ni kuongeza uzalishaji na usalama wa
chakula,” alisema Ismail Ngolinda kwenye Maonesho ya Nanenane
yanayoendelea kwenye Viwanja vya Ngongo mjini hapa.
Alisema mbegu hiyo licha ya kustahimili ukame, lakini pia in a
ukinzani dhidi ya bungua. Ngolinda aliongeza kuwa mradi wa WEMA umefanya
utafiti mbegu 11 chotara ambazo zinastahimili ukame. Alisema utafiti wa
mbegu hizo umefanywa kwa teknolojia ya kati.
Mtafiti huyo aliongeza kuwa mbegu hiyo inaweza kustahimili na kustawi
katika maeneo yenye mwinuko kati ya mita 0 hadi mita 1,500 kutoka usawa
wa bahari. “Maeneo ya Nyanda za Juu Kusini kwa kuwa kuna mwinuko mkubwa
mbegu hizi hazistawi, ila maeneo mengine ya nchi mbegu hizi zinastawi,”
alisema.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment