Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Dk Kalemani ameyasema hayo leo katika kijiji cha Mbwande wilayani Kilosa wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa awamu ya tatu ya mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na mamlaya ya Umeme Vijijini (REA).
Amesema watu hao maarufu kama vishoka, bado wamekuwa tishio kwa wananchi kwa kuwarubuni na kutaka kuwafanyia kazi za kuweka mfumo wa umeme majumbani wakiwatoza fedha nyingi na baadaye lawama kubaki kwa Tanesco.
Naibu Waziri huyo amewaagiza viongozi wa Tanesco, wakiwemo mameneja wa mikoa na wilaya, kuhakikisha wanatekeleza na kusimamia usaliji wa wakandarasi hao mara moja huku akieleza kuwa baadhi ya mikoa imeanza zoezi hilo.
“Kwa mkoa wa Morogoro, kwa taarifa zilizopo ni wakandarasi 17 pekee ndio waliosajikliwa na kutambulika. Hivyo ni vyema wananchi wakawatumia ili kuepuka kuibiwa na vishoka,”amesema Dk Kalemani.
Akizungumzia mradi wa REA, Dk Kalemani amewataka wenyeviti wa halmashauri kupitia mabaraza ya halmashauri kuhakikisha wanapanga bajeti kwa ajili ya kufanya wiring kwenye zahanati, vituo vya afya, shule na magereza kwani ni kazi yao na si kazi ya wizara au Tanesco.
Amesema kazi ya mradi huo ni kuhakikisha umeme unasambazwa katika maeneo yote ya vitongoji na vijiji nchini, taasisi za serikali,na mashirika ya dini hadi kufikia 2021 ambapo mpaka kukamilika kakwe unatarajiwa kutumia zaidi ya shilingi 45.34 bilioni.
Ametaja kuwa katika awamu hiyo ya tatu, zaidi ya vijiji 150 vinatarajiwa kupatiwa umeme mkoani Morogoro huku vijiji 26 tu vikibakia, a kwamba serikali imedhamiria kutatua changamoto za umeme za kuwafanya wananachi kuacha kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kufata huduma kwa ajili ya malighafi zao kama mazao.
Mkurugenzi mkuu wa mradi wa umeme vijijini, Gissima Nyamohanga, alieleza kuwa mpango wa serikali ni kuhakikisha kuwa umeme umefika katika vitongoji, vijiji, kata na wilaya ifikapo mwishoni mwa mwaka 2021 na kazi itakayobaki ni kuyafikia maeneo mapya.
Nyamohanga amesema umeme umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa viwanda kwa wananchi na Tanzania kwa ujumla kwani ndio tegemeo kubwa katika uzalishaji hasa kilimo.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji kwa wateja kutoka Tanesco makao makuu, Joyce Ngahyoma, amesema jukumu la Tanesco ni kuhakikisha maeneo ambayo mdumo wa umeme zimepita ni kulazimisha kushusha transifoma ili wananchi waweze kupata huduma.
Chanzo Mwananchi
Chanzo Mwananchi
0 comments:
Post a Comment