Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Afisa wa NSSF Mr Shaban Salehe akimwandikisha mwanachama
mpya katika banda la NSSF katika maonyesho ya Nanenane
yanayoendelea mkoani Morogoro.
Afisa
wa NSSF, Mwanawetu Njozi (kulia) akiongea na mgeni alietembelea banda
la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.
Afisa
wa NSSF, Jonathan Mkahala akimwandikisha mwanachama mpya katika banda
la NSSF katika maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro,
Pembeni kushoto ni Afisa mwandamizi wa Matekelezo wa Shirika hilo, Bw.
Salawa.
Afisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mbaga
akizungumza na wageni walietembelea banda la NSSF katika
maonyesho ya Nanenane yanayoendelea mkoani Morogoro.
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki maonyesho ya
Kilimo yanayoendelea mkoani Morogoro, Katika maonyesho hayo
wakazi wote wa Morogoro Hususan Wakulima wanakaribishwa
kupata elimu kuhusu namna ya kushiriki kilimo cha miwa
(Outgrowers Scheme) Mpango huu umeanziishwa mahususi ili
kuwasaidia watanzania kupata kipato kwa kulima miwa na Miwa
hiyo itanunuliwa moja kwa moja na Kampuni Hodhi ya Mkulazi
ambayo ni ubia kati ya NSSF na PPF.
Vile vile wananchi wote
wanakaribishwa kujiandikisha na NSSF ili kupata Matibabu bure
kwa mwanachama na wategemezi wake pamoja na Mafao
mengine yatolewayo na NSSF kama vile Mafao ya uzazi, kuumia
kazini, Mafao ya urithi, Pensheni ya uzeeni na mengineyo
0 comments:
Post a Comment