Mkurugenzi
wa Idara ya Mazingira -Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi
akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua warsha ya mafunzo ya kemikali na taka
hatarishi kwa mazingira kwa Maafsa sheria na maafisa Forodha. Warsha
hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais inafanyika mjini Morogoro.
Mgeni
Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bwana Clifford
Tandari akifungua Warsha ya mafunzo ya kemikali na taka hatarishi kwa
mazingira kwa Maafisa Sheria pamoja na Maafsa Forodha na Wakaguzi wa
mazingira na ubora wa bidhaa . Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya
Makamu wa Rais.
Sehemu
ya Wadau waliohudhuria warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa
Rais juu ya kujenga uelewa kwa Maafisa Sheria, Maafisa forodha na
Wakaguzi wa mazingira na ubora wa bidhaa kutoka Taasisi za Serikali
Mmojawapo wa watoa Mada katika warsha hiyo Bwana Faraja Ngerageza kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiwasilisha mada.
Mgeni
Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika picha ya
pamoja na Washiriki wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa
Rais inayofanyika mjini Morogoro.
Mgeni
Rasmi katika warsha hiyo Bwana Clifford Tandari pamoja na Mkurugenzi wa
Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kulia)
wakimsikiliza Mwakilishi wa WWF Africa Bwana Patrick Chibada wakati wa
Warsha hiyo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bwana Clifford Tandari amesisitiza kuwa ni
muhimu kujenga uelewa kwa Maafisa Sheria, Maafisa forodha na wakaguzi wa
mazingira na ubora wa viwango Nchini ili waweze kutambua kemikali na
taka hatarishi kwa mazingira na matumizi ya Binadamu. Ameyasema hayo
mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku tatu iliyoandaliwa
na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Aliongeza
kuwa moja ya changamoto ambayo dunia inaikabili kwa sasa ni usimamizi
wa kemikali na taka hatarishi katika jamii zetu. ” Hizi kemikali na
taka zinahitajika kusimamiwa vizuri ili kupunguza madhara ya afya kwa
binadamu na mazingira na pia Wanawake na watoto wapo kwenye hatari kubwa
ya kuathirika na kemikali hizo na kupeleka magonjwa makubwa hatarishi
yatokanayo na kemikali hizo” alisema.
Bwana
Tandari aliwataka Maofisa walioalikwa kujengewa uelewa wa kemikali na
taka hatarishi wakaitumie elimu hiyo katika majukumu ya kazi zao za kila
siku na hivyo kupelekea usimamizi stahiki wa wa taka na kemikali hizo.
Na hiyo itapelekea kupunguza na kumaliza kabisa athari za kemikali na
taka hatarishi katika Nchi yetu.
Warsha
hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira ili
kuwajengea uelewa Maafisa hao ili kuweza kudhibiti uingizwaji na
usambazaji wa kemikali hizo hatarishi Nchini. Katika Warsha hiyo Maafisa
wa forodha, sheria na wakaguzi wa Mazingira na viwango vya ubora
wamehudhuria hivyo basi uelewa juu ya kemikali hizo utaongezeka na
utawasaidia katika majukumu yao ya kila siku wanapokua makazini.
0 comments:
Post a Comment