Askofu Thelesphor Mkude wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro
WAAJIRI nchini wameaswa kutafuta njia za kuboresha maslahi kwa
wafanyakazi wao, badala ya kuwalipa mshahara mdogo kwa kuendekeza
maslahi binafsi.
Rai hiyo ilitolewa na Askofu Thelesphor Mkude wa Kanisa Katoliki
Jimbo la Morogoro, baada ya kufungua mkutano mkuu wa nne wa Chama cha
wafanyakazi Wakatoliki Tanzania (CWM), uliofanyika katika parokia ya
roho mtakatifu kiwanja cha ndege Mjini hapa.
Alisema licha ya wafanyakazi kutumia juhudi zao katika kazi
mbalimbali, baadhi ya waajiri huwalipa mshahara mdogo na wakati mwingine
kuwacheleweshea.
Aidha, alisema waajiri watafute upeo na utajiri wao lakini wasisahau
kuwa wafanyakazi wao wanapaswa kulipwa inavyostahili kadri ya mapatano
yao na kwamba lazima mapatano hayo yalingane na kima cha serikali.
Alisema kila mtu anapenda kufanya kazi ili apate mapto tena halali
ambapo. Alieleza kuwa baadhi ya waajiri wanapenda kuwanyonya wafanyakazi
wao kwa kutowalipa mishahara wanayostahili.
“Haiwezekani mtu mmoja akajitayarisha kwa kuwanyonya wengine kwa
kutowalipa mishahara wanayostahili, ni bora kama hawezi afunge kiwanda
chake,”alisema Mkude Alisema kuwa wengine wanapotaka kupata faida huwa
hawaangalii njia ya kupata faida.
Chanzo Na Habari Leo
0 comments:
Post a Comment