Wilaya ya
Kilindi Mkoani Tanga haina Ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo
wanapohitaji huduma mbalimbali zinazohitaji kuwezeshwa na TRA.
Akizungumza
Bungeni Mjini Dodoma wakati akiuliza swali kwa serikali Mbunge wa
Kilindi Omary Kigua (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itafungua
ofisi ya wilaya ili wananchi waweze kulipa mapato kwa urahisi kuliko
ilivyo sasa.
Akijibu
sali hilo Naibu Waziri wa Fedha Bi. Ashanti Kijaji amesema serikali
inatambua umuhimu huo wa kuanzisha ofisi hiyo lakini kwa sasa kipaumbele
kipo katika mikoa mipya iliyoanzishwa.
Aidha naibu
Waziri amewataka wananchi wa Kilindi kuendelea kulipa kodi wakati
serikali ikiendelea na mchakato wa kufanya upembuzi wa kubaini gharama
za kuanzisha ofisi hiyo na vyanzo vitakavyo changia kuongeza mapato
wilayani Kilindi.
0 comments:
Post a Comment