Kampuni ya mawasiliano ya Smile Tanzania leo imezindua huduma zake za mtandao wake wa kasi kwa matumizi ya binafsi,wafanya biashara waliopo ndani na jirani na Mkoa wa Morogoro.
Akizungumza wakati wa hafla
fupi ya uzinduzi mkoani Morogoro, Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya
Smile Tanzania, Bw. Eric Behner amebainisha kuwa kampuni yake inatoa huduma
zenye kasi zaidi na kuaminika kwa wateja wake nchini Tanzania kupitia mtandao
wa 4G LTE kwenye wigo wa 800MHz yenye kasi ya kufikia mpaka 21Mbps.
“Smile imetumia tekinolojia na
viwango vya hali ya juu vya mawasiliano vilivyopo katika kutimiza ahadi yake ya
kutoa vifurushi vya intaneti vyenye kasi ya aina yake, ubora mkubwa, mtandao wa
kuaminika unaotumia vifaa rahisi kutumia na kufanya mapinduzi makubwa ya namna
watu wanavyoweza kuzifikia huduma za intaneti.” Alisema Bw. Behner
“Tunayo furaha kubwa kuleta
tekinolojia ya mtandao wa kisasa kwa wakazi wandani na jirani mkoaniMbeya.Tuna
uhakika wa kwamba upatikanaji wa intaneti yenye kasi utasaidia kwa kiasi
kikubwa mafanikio ya kibiashara na watu binafsi hapa mkaoni na nifaraj kubwa
kwetu kuwa sasa kila mtu hapa Mbeya sasa atajionea na kujivunia mwenyewe
mtandao huu kuwa ni wa uhakika na wenye huduma za gharama nafuu.” Aliongezea
Bw. Behner
Kampuni ya Smile pia imeleta
huduma ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wafanya biashara wa mkoani Mbeya,
ambapo kutakuwa na kiungio maalumu cha wigo mpana wa mtandao na kuyawezesha
makampuni yenye upungufu wa kuwasiliana na wafanyakazi ambao wako nje ya ofisi
kwa sababu moja au nyingine, basi itawaongezea uwezo wa kuzalisha na kupunguza
gharama za uendeshaji.
Katika sekta ya mawasiliano nchini Tanzania hivi sasa huduma ya
mtandao wa intaneti ya Smile ndiyo inayoongoza kwa kuwa na kasi ambayo ni mara
kumi zaidi ya ile ya 3G.Wateja sasa watajionea intaneti yenye kasi zaidi,
hususani wakati wa kupakia mafaili makubwa, kutuma barua pepe zenye
viambatanisho vikubwa, pamoja na kupakua mafaili, muziki, filamu na michezo ya
mtandaoni. Vilevile kupata huduma mbalimbali za kimtandao kama vile; kwa
kutazama video au luninga mtandaoni bila ya kukwama au kufunguka kwa muda
mrefu.
“Tunajivunia kwa kweli kuwaletea huduma ya intaneti yenye kasi
zaidi mkoani Mbeya ambayo ni sawa na ile yenye kasi na ubora wanayoifurahia
wenzetu wa Ulaya. Smile hatutoi huduma ya intaneti pekee, bali tutatoa huduma
ya intaneti yenye kasi zaidi, kuaminika wakati wote na yenye gharama ambayo
kila mtu ataweza kuimudu na pia tumejizatiti katika kuwaridhisha wateja wetu
kwa kiwango cha hali ya juu.” Alisisitiza Bw. Behner
Mikoa mingine ambayo tayari huduma ya Smile zinapatikana na inatarajiwa
kunufaika na huduma hizi ni Dar Es Salaam,Mwanza,Mbeya,Arusha,Kilimanjaro naDodoma.Smile
inatarajia kuendelea kujipanua kwenye mikoa mingine Katika huduma za 4G LTE.
Baada ya uzinduzi huo, kampuni
ya mawasiliano ya Smile Tanzania imewataka wakazi wa mkoani Morogorona maeneo
ya jirani kutembelea duka lao li kujaribu na kushuhudia kasi ya mtandao huo
ulio wa ajabu au kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja kwa kupiga simu
namba 0662 100 100.
Imetolewa na;
Linda Chiza
Smile Communications Tanzania
Kwa niaba ya:
0 comments:
Post a Comment