Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Serikali
imetoa siku saba kwa kiwanda cha sukari cha Mtibwa kulipa faini ya
shilingi milioni 50 baada ya kudaiwa kukiuka sheria za mazingira.
Baadhiya
mambo yaliyobainika ni kukosa mfumo mzuri wa kuhifadhi na kusafirisha
taka ngumu na taka maji, kutohifadhi vyema kemikali zinazotumiwa na
kiwanda hicho pamoja na kutumia kuni kuendesha baadhi ya mitambo yake
hususani eneo la kuchemshia.
Uamuzi
huo umefikiwa baada ya kufanywa kwa ziara ya kushtukiza kiwandani hapo
na naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira
Luhaga Mpina, aliyeambatana na wataalamu kutoka baraza la taifa la
hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC).
Mh
Mpina amesema tayari serikali ilishakataza viwanda kutumia kuni na
magogo kuendeshea mitambo yake, huku akitoa siku 30 kwa uongozi wa
kiwanda hicho cha Mtibwa kufanyia marekebisho mapungufu yote yaliyotajwa
vinginevyo serikali itakifunga.
Akiwa
kiwandani hapo naibu waziri Mpina amewaagiza viongozi wa mamlaka
mbalimbali kuwajibika katika agizo la usafi wa mazingira kwa kila
Jumamosi ya mwisho wa mwezi sambamba na kuwaagiza wakurugenzi wa
halmashauri za wilaya kuhakikisha miti milioni 1.5 inapandwa kila mwaka.
Kaimu
meneja mkuu wa kiwanda cha sukari Mtibwa Ahmad Yahya pamoja na kuridhia
maagizo yaliyotolewa, ameiomba serikali kuwapunguzia faini hiyo ya
shilingi milioni 50 ambayo amedai kuwa ni nyingi kwa kiwanda hicho
kumudu
0 comments:
Post a Comment