Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Mkuu wa Wilaya Morogoro ameagiza polisi kuwakamata wanakijiji wa Kisaki Stesheni waliohusika na mapigano kwa kutumia silaha za jadi jana tarehe 20/01/2016 katika mkutano wa hadhara uliyolenga kutoa ufafanuzi wa mgogoro huo.
Mkuu
wa Wilaya Bw.Muhingo Rweyemamu ameyasema hayo leo alipokuwa akizunguza
kwa njia ya simu alipohitajika kutoa ufafanuzi kuhusu tukio la uvunjifu
wa amani kwa wanajikiji hao waliyokuwa na Mgororo wa ardhi unaowahususha
wakulima na wafugaji.
“Mgogoro huu wa Ardhi umesababishwa na Mwenyekiti wa Kijiji Bw. Ismail N’ganji kwani aligawa ardhi hiyo ya kijiji mara mbili kwa wakulima na wafugaji wakati katika taratibu
za kugawa ardhi ni lazima wanakijiji waamue katika kikao cha kijiji, na
maombi ya kuomba ardhi ya Kijiji cha Kisaki yalikuwa kati ya wakulima
na wafugaji ambao
kijiji kiliadhimia kuwa ardhi hiyo ipewe wafugaji ambapo Mwenyekiti wa
Kijiji aliamua kugawa ardhi hiyo kwa wakulima kinyume na makubaliano ya
Mkutano wa Kijiji na hapo ndipo chanzo cha mgogoro huo ulipoanza”,
alisema Bw.Rweyemamu.
Mbali
na hayo Bw. Rweyemamu alisema mpaka sasa mwenyekiti huyo wa kijiji
ameshafukuzwa na uchaguzi wa Mwenyekiti mwingine unatarajia kufanyika
hivi karibuni nakuwataka viongozi wa kijiji kuzingatia sheria za ugawaji
ardhi na kuacha kukiuka misingi hiyo kwani ndiyo inayosababisha
migogoro mingi ya ardhi katika maeneo mbalimbali.
Akiendelea
kuzungumza mkuu huyo wa wilaya alisema sheria ya ardhi inaeleza vizuri
endapo mtu atahitaji ardhi isiyozidi heka 50 basi ni lazma awasilishe
maombi hayo kwa mkuu wa wilaya na wanakijiji wahusishwe katika kikao cha
maamuzi ya kuridhia na kwa upande wa mtu atakayehitaji ardhi Zaidi ya
heka 50 basi maombi yatatakiwa kuwasilishwa kwa Waziri wa Ardhi Nyumba
na Makazi.
Hata
hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo alisema Migogoro ya ardhi imekuwa
inasababishwa na viongozi wa kijiji kwa kiasi kikubwa kwani baadhi yao
wamekuwa wakiendekeza rushwa huku wakisababisha uvunjifu wa Amani kwa
wanakijiji hivyo wito wake ni viongozi hao wazingatie maadili ya
kiutendaji na kuachana na vitendo vya rushwa.
0 comments:
Post a Comment