Home » » TFDA: IMEFUTA USAJIRI WA AINA ZA DAWA ZA BINADAMU AINA TANO NA KUAMURU ZIONDOLEWE SOKONI NA VITUO VYA AFYA NCHINI.

TFDA: IMEFUTA USAJIRI WA AINA ZA DAWA ZA BINADAMU AINA TANO NA KUAMURU ZIONDOLEWE SOKONI NA VITUO VYA AFYA NCHINI.

 
Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA imefuta usajiri wa aina za dawa za binadamu aina tano na kuamuru ziondolewe sokoni na vituo vyote vya kutolea huduma za afya mchini kote mara moja kutokana na kubainika kuwa na viambata vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na wakati mwingine kusababisha vifo.
Dawa zinazotajwa kufutiwa usajiri na kuzuia uingizwaji kuwa ni pamoja na dawa za kutibu maralia ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine, dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsulis zenye kiambata cha Fenil Propanolamine nyingine ni dawa ya sindano aina ya Chrolaphenical inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln cha nchini India, dawa za kutibu fungus ya vidinge na kapsuli.
 
Akitangaza dawa hizo mkurugenzi mkuu mamlaka ya chakula na dawa TFDA Bw. Hiit Sillo hatua hiyo imefikiwa baada ya uchuguzi wa kitaalam wa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO.
 
Aidha TFDA imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya maralia ya SP kutumika kama kinga ya maralia kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza watengenezaji kubadili machapisho na vifungashio vyake mara moja ambapo mkurugenzi wa dawa TFDA Bw. Mitanga Fimbo pamoja na kufafanua athari anawataka watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza mara moja kabla ya kuanza kwa msako.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa