Home » » WAFUGAJI WAENDELEA KUVAMIWA NA MADEREVA WA BODA BODA NA KULAZIMIKA KUKIMBIA MJI WA MOROGORO.

WAFUGAJI WAENDELEA KUVAMIWA NA MADEREVA WA BODA BODA NA KULAZIMIKA KUKIMBIA MJI WA MOROGORO.

 
Hofu imeendelea kutanda kwa wafungaji mkoani Morogoro kufuatia bodaboda kuendelea kuwavamia na kuwapora wafugaji kila wanapoonekana katika mji wa Morogoro kwa madai ya kulipiza kisasi baada ya mkulima mmoja kuuwawa katika bonde la mgongola ambapo   wafanyabiashara wafugaji na wanaofanya shughuli za ulinzi   wamelazimika kuukimbia mji wa Morogoro na baadhi ya wanafunzi wa vyuo na kurudi majumbani.
Wakizungumza wakiwa porini kujadili hatma ya usalama wa wafugaji  hao wakiwemo wanaume kwa wanawake kutoka wilaya za Kilosa na Mvomero wamesema hawakuusika na mgogoro uliosababisha mauaji ya mkulima katika bonde la mgongola na hivyo kuomba serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama wawasaidie  kwani hivi sasa wagonjwa wanalazimika kutibiwa majumbani wanafunzi hawaendi shule kwa kuhofia madereva wa bodaboda.
 
Nao baadhi ya wafugaji waliojeruhiwa na kuporwa fedha wameeleza jinsi walivyovamiwa na kupigwa kisha kunyanganywa simu na fedha na hivi sasa wanaugulia majumbani na wanashindwa kwenda hospitali kupata matibabu kwa hofu ya kuvamiwa na madereva wa bodaboda huku baadhi ya wanafunzi wafugaji wanaosoma chuo cha St Josefu Morogoro nao wameelezwa kurudi majumbani.
 
Wakati haya yakitokea jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewafikisha mahakamani madereva wa boda boda 11 waliobainika kuhusika na matukio ya kuvamia wafugaji ambapo wamesomewa mashataka mawili ya kuvamia wafugaji kwanyakati tofauti mbele ya hakimu mkazi Maua Hamduni ambapo washtakiwa wamenyimwa dhamana kwa hofu ya usalama wao na kurudishwa rumande .
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa