Rais
wa shirikisho la soka nchini TFF Gamal Malinzi amesema siku miamoja za
uongozi wake katika shirikisho hilo amekutana na changamoto nyingi
ikiwa ni pamoja kukuta madeni mengi pamoja na mikataba isiyokuwa na
tija.
Ukisoma kitabu cha pili cha mwandishi Nguli Leroy
Brownlow utabaini kuwa mwandishi alitaka kuiaminisha jamii kiongozi
anayependwa na umma anaweza kuleweshwa na upendo huo na akasahau
kutekeleza ahadi rais wa TFF Gamali Malinzi akiwa na siku 100 tu ofisini
kwake anaweza kusoma kitabu cha Lery Brownlow kama kinamuhusu ama laa
kisha akajipima.
Akielezea siku 100 alizokaa katika kiti hicho
malizni amesema amefikia malengo alotaraji lakini amekuwa akivutwa shati
kurudi nyuma na baadhi ya maswala ikiwa ni pamoja na kukuta madeni
mengi yaliyoachwa na utawala uliyopita.
Malinzi pia amezungumzia udhia wa tiketi za
kieletronick huku akijitoa kuwa mtaka huo ameukuta na una kasoro nyingi
ingawa ina nia njema.
Siku miamoja za unahodha wake katika jahazi la soka
nchini Tanzania pamoja na jitihada za dhahiri anazoonyesha katika
kukuza soka nchini pia amekumbwa na kadhia za kudekeza ukabila hasa
kanda ya ziwa jambo analolikanusha vikali kama alivyokanusha leo.
Chanzo:ITV Tanzania
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment