Home » » WATAALAMU WATAFITI PANYA VIJIJINI

WATAALAMU WATAFITI PANYA VIJIJINI

CHUO kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro kwa kushirikiana na wataalamu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) wameanzisha maabara za utafiti wa vimelea vilivyo kwenye panya vijijini.

Maabala hiyo inayokwenda sambamba na kufanya upasuaji wa panya unalengo kuongeza kasi ya tafiti mbalimbali kwenye panya hao na kubaini aina mbalimbali za vimelea walio kwenye panya na athari zake kwa binadamu.

Mtafiti kutoka SUA, Profesa Rhodes Makundi, alisema mbali na utafiti huo unaoshirikirikisha watafiti wengine kutoka nchini za
SADC ujulikanao kama ECORAT pia unalenga kutafuta njia mbadala ya kupambana na panya waharibifu wa mazao badala ya kutumia madawa yenye mchanganyiko wa kemikali za viwandani.

Tayari upasuaji huo umeanza katika Kijiji cha Berega, wilayani Kilosa ambapo watafiti hao wanaoshirikiana na watafiti toka nje ya nchi tayari wamebaini magonjwa mbalimbali hatari kwa afya za binadamu.

Alitaja magonjwa yaliyobainika kuwa ni ugonjwa wa tauni, homa ya laso ambayo yakikosa tiba mapema yanaweza kusabisha vifo kwa binadamu.

Aidha, athari nyingine kutokana na takwimu za tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania hupoteza zaidi ya tani 400,000 za mahidi yanayoharibiwa na panya; tani hizi ni sawa na asilimia 15 ya fedha za kigeni zinazokadiriwa kuwa na thamani ya dola 40,000 zinazoweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo.

Mradi huo umeanzia katika vijiji vya Berega Tarafa ya Gairo, Wilaya ya Kilosa kutokana na eneo hilo kuathirika zaidi na panya
 Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa