Home » » ABOOD ATOA MSAADA KWA WAJASIRIAMALI

ABOOD ATOA MSAADA KWA WAJASIRIAMALI

 Abood atoa msaada kwa wajasiriamali
 MBUNGE wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ametoa misaada ya vifaa vya ujenzi na fedha kwa vikundi vya wajasiriamali 15 vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 17.5 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi.
Akikabidhi misaada hiyo jana, mbunge huyo alisema inalenga kusaidia sekta za elimu, maji, afya, umeme, uchumi na huduma nyingine za kijamii.
Misaada hiyo inajumuisha matofali 5,000 kwa ajili ya Msikiti wa Kihonda Maghorofani, mbao 200 kwa Msikiti wa Legezamwendo Kata ya Kingolwira, mifuko 120 ya saruji kwa ajili ya Shule ya Awali na Msingi ya Agap na karavati kwa ajili ya kukarabati barabara za Kata ya Mafisa.
Vingine ni tangi la maji la lita 5,000 na hundi ya sh 300,000 kwa vikundi vya ujasiriamali vya Silc, sh 500,000 kwaya ya Mtakatifu Peter na sh 400,000 kwa kikundi cha kina mama wa Agape cha Bigwa.
Alisema ataendelea kusaidia wananchi wa jimbo hilo kila mahali penye uhitaji.
Katika sekta ya maji, Abood alisema tayari ameshajenga visima 21 vyenye thamani ya sh milioni 365 na kati ya hivyo, vinne havijaanza kutoa maji kutokana na hali ya ukame ya mahali ambako vilichimbwa.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa