MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesema vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike bado ni tatizo nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi alisema hayo kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.
Alisema licha ya juhudi mbalimbali za kupambana na ukatili wa kijinsia nchini, bado hali ni mbaya.
Aidha akizungumzia ndoa za utotoni, alisema takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, zinaonesha katika mwaka 2013 asilimia 23 ya wasichana wenye umri kati ya miaka 15 na 19 walikuwa na ujauzito au na watoto.
Alisema katika kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mwaka huu, TGNP imeandaa mjadala wa wazi utakaofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Chanzo;Habari Leo
0 comments:
Post a Comment