Halmashahuri ya Manispaa ya Morogoro, kwa kushirikiana na Chuo
cha Ufundi Stadi (Veta), inakusudia kuanzisha mpango maalumu wa elimu
kwa wajasiriamali wadogo wenye lengo la kuwawezesha kupata maarifa ya
kuendesha biashara zao kwa tija.
Elimu hiyo pia inalenga kuwawezesha washiriki kujua mbinu za kupata mitaji kutoka katika taasisi mbalimbali za fedha.
Hayo yalisemwa jana na meya wa Manispaa ya
Morogoro, Amir Nondo alipokuwa akizungumza na wanachama wa kikundi cha
Vikoba Mshikamamo ‘B’.
Nondo alisema mpango huo umekuja baada ya
kubainika kuwa wajasiriamali wengi wanafanya biashara zao bila elimu ya
biashara, hali inayowafanya washindwe kupiga hatua.
Meya huyo alisema elimu ya biashara inahitajika
kwa wajasiriamali hasa katika kipindi hiki ambacho kina ushindani mkubwa
wa bidhaa sokoni.
“Ndiyo maana tumeamua kuwasaidia wajasiriamali
kupata elimu nao waendeshe biashara zao kwa umakini zaidi kuliko ilivyo
sasa,” alisema.
Kwa upande wake, mwenyekiti wa Vikoba Mshikamano
‘B’, Sauda Juma alisema wanachama wake wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kikundi kutokuwa na mtaji wa kutosha
kuweza kukopeshana kiwango kikubwa cha fedha.
“Hii ni changamoto inayotusumbua, tunawaomba wadau wajitokeze kutusaidia kukuza mtaji wetu,” alisema.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment