Home » » MBUNGE AWAPA SOMO WAZAZI

MBUNGE AWAPA SOMO WAZAZI

MBUNGE wa Morogoro Mjini, Aziz Abood ametoa mwito kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanatenga fedha za mahitaji ya watoto wao na kuacha tabia ya kutumia fedha bila uangalifu.
Rai hii aliitoa juzi akisema wazazi wasiendekeze sikukuu kwa jambo ambalo husababisha watoto wengi kubaki nyumbani kutokana na wazazi kushindwa kulipa ada baada ya kutumia fedha nyingi katika kipindi cha sikukuu.
Abood alisema kuwa vijana wengi wamemaliza darasa la saba mwaka huu na wamefaulu na kupangiwa shule hivyo ni jukumu la wazazi kuhakikisha watoto hao wote wanaendelea na elimu ya sekondari.
“Sitegemei kuona mtoto hata mmoja ndani ya manispaa akabaki nyumbani kwa kisingizio cha kukosa ada,” alisema.
Aidha, alisema kuwa jamii inapaswa kukumbuka majukumu ya mbeleni na sio kuishia kusherehekea kwa kula na kunywa na kusahau elimu ambayo ndio ufunguo wa maisha ya watoto wao.
Alisema wazazi wamekuwa na tabia ya kusahau wajibu wao wa kuwapatia watoto elimu na hatimaye hujikuta wakiishia kwanunua nguo za sikukuu na kufanya matumizi yasiyo ya lazima na kusahau kama kuna kulipa ada ya mtoto katika mwakani unaofuata.
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa