Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro,
(Kushoto), akizungumza na baadhi ya wajumbe wa idara ya utumishi wa
walimu, kwenye eneo la mradi wa nyumba za Mfuko huo eneo la Lukobe mjini
Morogoro mwishoni mwa wiki. Wajumbe hao walifanya ziara hiyo mara baada
yab kuhudhuria semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa lengo
la kuwaelimisha juu ya faida mwanachama anazoweza kupata anapojiunga na
Mfuko huo.
Mkurugenzi wa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Neema Muro,
(Kushoto), akiwapa maelezo, baadhi ya wajumbe wa tume ya utumishi wa
walimu, kuhusu mradi wa nyumba za Mfuko huo, zilizoko eneo la Lukobe
mjini Morogoro, mwishoni mwa wiki.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi,
(Mwenye T-Shirt), akiwapa maelezo wajumbe wa idara ya utumishi wa
walimu, kuhusu nyumba za Mfuko huo zilizoko eneo la Lukobe mjini
Morogoro, mwishoni mwa wiki mara baada ya kuhudhuria semina ya siku moja
iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini humo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment