Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VIJANA kutoka vijiji 20 vinavyozunguka hifadhi ya taifa ya Mikumi Kilosa mkoani Morogoro wameshauriwa kuacha mara moja kujihusisha na vitendo vya ujangili na badala yake kuunda vikundi vidogo vya ujasiriamali ili wapewe fursa za mikopo.
Rai hiyo imetolewa juzi na Mbunge wa Mikumi, Abdusalaam Sas, wakati akizindua tamasha la kupiga vita ujangili na mauaji ya tembo, lililoandaliwa na mtandao wa habari za kijamii Tanzania (Mhakita), chini ya ufadhili wa Tanapa.
Mbunge huyo, alisema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya ujangili katika maeneo mengi sasa hivi kutokana na baadhi ya watu kujihusisha na biashara haramu ya pembe za ndovu na nyama pori.
Aidha, alisema kuwa kijana wa kitanzania kujihusisha na vitendo vya ujangili ni kukosa uzalendo ndani ya nchi yao kwa kushiriki kufanya uhujumu.
Hata hivyo, alisema kama mbunge yupo tayari kusaidia vikundi vya vijana mitaji ili waweze kuacha kujiingiza katika matukio ya ujangili.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment