Home » » SHIMIWI YAZIDI PAA

SHIMIWI YAZIDI PAA



Hoi hoi na nderemo zimepamba moto katika viwanja mbalimbali mkoani Morogoro wakati watumishi wa umma wakioneshana utaalamu katika michezo mbalimbali wakati wa mashindano ya SHIMIWI inayoendelea mjini Morogoro.
Ndermo hizo zimeonekana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo ilipofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali mpira wa miguu kwa kuwatoa Wizara ya maji kwa njia ya matuta katika mchezo uliochezwa katiak nyasi za uwanja wa Mazimbu mjini Morogoro.
Mchezo huo uliisha kwa timu hizo kufungana bao 1-1 ambapo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Wizara ya Maji dakika ya 21 kipindi cha kwanza kwa goli lililofungwa na James Mapepe wakati goli la kusawazisha la Wizara ya Maji lilifungwa kipindi cha pili na mchezaji Alifa Ismail katika dakika ya 40 ya mchezo.
Baada ya dakika 60 za mwamuzi wa mchezo huo Baraka Rashidi, timu hizo zilikuwa na goli moja kila mmoja hivyo mwamuzi huyo kwa kufuata kanuni na taratibu za mashindano hayo aliamuru matuta yapigwe ili apatikane mshindi.
Mlinda mlango wa timu ya likuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaaduni na Michezo Ramadhani Mtenga ndiye aliyeibuka kuwa shujaa wa mchezo kwa kupangua penati moja na kuipa timu yake ushindi wa penati 3 -1 dhidi ya Wizara ya Maji.
Mwamuzi wa mchezo huo alisaidiana na washika vibendera Erick Joseph na Ramadhani Sadick wakati kamisaa wa mchezo huo alikuwa Godifrey Evance wote wanatoka kituo cha kukuza vipaji vya michezo cha Twalipo Youth Foundation cha mjini Morogoro.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa