Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKULIMA wa Miwa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, ameibuka na utabiri kuwa zao hilo litakufa miaka miwili ijayo endapo serikali na wakulima nchini hawatakutana haraka na kuunda ajenda ya kulinusuru.
Akizungumza mjini hapa mwishoni mwa wiki, Guninita ambaye ni miongoni mwa wakulima wakubwa wa katika Bonde la Kilombero, alisema zao hilo tegemeo kubwa kwa wananchi na uchumi wilayani hapa litakufa kutokana na thamani ya miwa kushuka mwaka hadi mwaka.
“Mfano msimu uliopita wakulima tumeuza hadi sh 55,000 kutoka sh 67,000 kwa tani…sasa upo uwezekano mkubwa tukakimbilia kulima mpunga,” alisema.
Alibainisha kuwa, msingi mkubwa wa tatizo hilo la kushuka kwa bei ni watu binafsi kupitia mikono ya serikali, kuagiza sukari nyingi toka nje ya nchi na ongezeko kubwa la njia za panya mipakani.
Aidha, aliongeza kuwa sera ya kumlinda mlaji ina changamoto kubwa katika uboreshaji pato la mkulima wa miwa nchini, kwa kuwa sukari ya nje imekuwa ikilipiku soko la sukari ya ndani kutokana na tofauti kubwa ya bei ya bidhaa hizo.
“Nadhani jukumu la kuagiza sukari nje ya nchi lipewe wenye viwanda ili wadhibiti kikamilifu uchakachuaji na kuongeza tija kwa mkulima wa nadani badala ya mfumo wa sasa, kwani unawaumiza wakulima hasa wadogo,” aliongeza.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment