Home » » SERIKALI YAOMBWA RUZUKU SKAUTI

SERIKALI YAOMBWA RUZUKU SKAUTI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SERIKALI imeombwa kutenga bajeti maalumu itakayotolewa ruzuku kwa vijana Skauti nchini ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwaandaa kuwa na uzalendo.
Ombi hilo lilitolewa na Kamishina Mkuu Msaidizi Programu za VijanaSkauti, Mary Anyitike kwenye hafla fupi ya kutoa nishani kwa viongozi wa Skauti kituo cha Bahati Camp mjini hapa na kufunga mafunzo ya skauti kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Shinyanga, Pwani na Mbeya.
Kamishina huyo, alisema mbali na vijana kujitokeza kwa kiwango kidogo kushiriki mafunzo na shughuli za maendeleo, bado kuna changamoto ya kutokuwa na fungu la uendeshaji hasa katika kugharamia shughuli walizonazo.
“Kutokana na changamoto hiyo, imepelekea vijana na walimu wakufunzi kushindwa kushiriki kikamilifu katika ujenzi, hivyo tunaiomba serikali itoe ruzuku kwa skauti ili tuweze kuendelea kufundisha vijana,” alisema Anyitike.
Alisema kuwa lengo kuu la kutoa mafunzo hayo, ni kuwatengeneza vijana wakakamavu na wenye kuwa na uzalendo na nchi yao, sambamba na kujifunza stadi mbalimbali za kimaisha ikiwemo utunzaji mazingira.
Kwa upande wake, Mtahini Mkuu Bahati Camp, John Lusunike, alisema bado taaluma ya skauti iko chini huku akiwataka viongozi na wawakilishi kuhakikisha wanalifanyia kazi.
Awali, Flora Bernard, akizungumza kwa niaba ya wahitimu wenzake, alisema mafunzo hayo yameweza kuwakutanisha kwa pamoja na kusaidiana katika shughuli mbalimbali sambamba na kuimarisha afya zao na kuwa wakakamavu kupitia mazoezi mbalimbali.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa