Home » » MUME AUA MKE KWA WIVU WA MAPENZI

MUME AUA MKE KWA WIVU WA MAPENZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

NEEMA Sanga (33), mkazi wa Mngeta wilayani Kilombero mkoani hapa, ameuwawa nyumbani kwake kwa kucharangwa mapanga na anayedaiwa kuwa mumewe, Laurian Labani, kwa wivu wa mapenzi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, alisema tukio hilo lilitokea Septemba 25 saa 3 usiku, baada ya kuhitilafiana na kunyimana unyumba kwa muda mrefu.
"Inasemekana wapenzi hao walikuwa na ugomvi wa mapenzi ndani ya nyumba kwa muda mrefu na siku ya tukio, marehemu hakuwepo nyumbani, jambo lililomfanya mumewe kunoa panga na kuanza kumsaka kwa pikipiki sehemu mbalimbali," alisema Kamanda Paul.
Kamanda huyo, aliongeza kuwa kabla ya kuuwawa Neema alikatwa na panga shingoni, taya la kulia na kwenye paja, ambako alipiga kelele na watu kukusanyika lakini alifariki kabla hajapata msaada.
Wakati huo huo, jeshi hilo linawashikilia watu watatu akiwemo dereva Hassan Yasin, utingo Frank John wenye gari Mitsubishi Fusso namba T 703 AUY na Rashid Ramadhani ‘Duge’ (45), wa Doma Mvomero kwa tuhuma za kusafirisha bangi kwenda jijini Dar es Salaam.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa