Mradi wa miaka mitano wenye lengo la kubadili Sera,sheria
na taratibu zinazozuia kukua kwa sekta binafsi katika sekta ya kilimo
umezinduliwa rasmi hivi karibuni.Mradi huo unaogharamiwa na Taasisi ya
mapinduzi ya kijani barani Afrika umezinduliwa na Mkurugenzi wa masuala
ya Sera na mpango wizara ya kilimo,chakula na ushirika Mkuvilwa
Simkanga.
Mkurugenzi huyo amesema mradi huo umelenga kuipatia wizara yake uwezo wa kubadili mwenendo wa sekta ya kilimo kwa kuwa na uhakika na tafiti kuhusu Sera,sheria na taratibu ili vyote hivyo viweze kutumika kuinua kilimo.
Amesema kwa kuwa mchangiaji mkubwa katika sekta ya kilimo ni sekta binafsi na kutokana na vikwazo mbalimbali vinakwamisha kukua kwa sekta ya kilimo kutokana na sheria mradi huo utawezesha kubainishwa kwa matatizo na kuyapatia ufumbuzi.
0 comments:
Post a Comment