Home » » MBUNGE WA JIMBO MOROGORO KUSINI ATEKELEZA AHADI YAKE YA KUKUWEZESHA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI‏

MBUNGE WA JIMBO MOROGORO KUSINI ATEKELEZA AHADI YAKE YA KUKUWEZESHA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI‏

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris (kulia) Ahimkabidhi Pikipiki 11 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar Ikiwa Ni ahadi yake aliyoitoa ya Kukusaidia chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.Mh Kalogeris Amekabidhi pikipiki hizo akiwa na Lengo Kila kata Kuwa na Pikipiki MMoja uwe Mradi wa Chama ili kuwezesha Kila kata Kuendesha Shuguli za Chama Bila kuwa wategemezi .Mbunge Kalogeris amehadi kuhakikisha kata zote za jimbo hilo zinapatiwa Pikipiki.Mh Kalogeris amesisitiza Pikipiki hizo ni mali ya CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini na si mali ya watu binafsi. 
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris  Akitoa hotuba yake Namna atakavyoshirikiana na Wanachama na Viongoizi wa Jimbo la Morogoro Kusini bega kwa bega ili chama hicho kiweze kujitegemea kiuchumi kwajili ya kutekeleza Majukumu yake ya Kila siku Ikiwemo Kushinda kwa kishindo Uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwaka 2O15.
Mwenyekiti wa CCM Morogoro Vijijini Mh Jazar akisisitiza jambo wakati akitoa neno la Shukrani mara Baada ya Kupokea Msaada ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini  Mh Kalogeris aaliyoitoa kwajili ya kukifanya Chama cha Mapinduzi Kujitegemea Kiuchumi.
 Wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Morogoro vijijini waliojitokeza wakati wa Kupokea Msaada huo. 



 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini Mh Jazar (Kulia) Akikabidi Pikipiki kwa Mmoja wa Mwakilishi wa kata zinazounda Wilaya ya Morogoro mjini Ikiwa kama mrdi wa kukiwezesha chama hicho kujitegemea Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa