Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI wa Tarafa ya Malinyi Wilayani ya Ulanga mkoani Morogoro,
wametaka kufahamu hatua zilizochukuliwa na Serikali baada ya mauaji ya
kupigwa risasi kwa raia yanayodaiwa kufanywa na askari watatu wa eneo
hilo.
Mauaji hayo yalifanyika wakati wa maandamano ya amani kupinga
unyanyasaji, ucheleweshaji wa kesi na uonevu uliokuwa ukifanywa kwao na
baadhi ya askari wa kituo hicho.
Kilio hicho kilitolewa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji
cha Malinyi ambapo mmoja wao, Protas Itema alisema wanashangazwa kuona
serikali iko kimya hadi sasa kufuatia mauaji hayo.
Mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Juma Mponda aliwataka wananchi hao
kuwa watulivu kwa vile aerikali imeshaanza kuchukua hatua ikiwemo
kufanya mabadiliko ya askari wa kituo cha polisi Malinyi.
Alisema kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao lakini hawataweza
kufanikiwa bila wananchi kuwapa ushirikiano ili kuwatia mbaroni
watuhumiwa wanaohusika na vitendo mbalimbali vya kiuhalifu, yakiwemo
mauaji ya mfululizo yaliyojitokeza.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment