Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI
wa Jimbo la Ulanga Magharibi mkoani Morogoro, wamemuomba Rais Jakaya
Kikwete kutimiza ahadi yake ya uchaguzi za mwaka 2010, ya kuwapatia
wilaya mpya kwa mipaka ya kimajimbo.
Walisema kuwa kwa hali inavyokwena sasa wakati huu muda ya Rais
Kikwete ukielekea ukingoni, baadhi ya watendaji na viongozi wa
kiserikali wanakwamisha mchakato huo kwa makusudi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano ya hadhara kwenye
vijiji na makao makuu ya tarafa nne za wilaya hiyo za Lupiro, Mtimbira,
Malinyi na Ngoheranga, baadhi ya wananchi hao, walidai kushangazwa na
ugumu unaojitokeza katika upatikanaji wa wilaya mpya wakati
walishamuomba Rais na akaahidi kuwapatia.
Kwa nyakati tofauti wananchi hao walibainisha umuhimu wa wilaya mpya
ili kusogeza huduma za kijamii na kiuchumi karibu, huku wale wa Minepa
wakimtuhumu diwani wao Athumani Kapati kuwashawishi kukubali Lupiro
iende Ulanga Mashariki.
Wananchi hao walidai kuwa wana hofu ya mchakato huo umeanza
kuingiliwa na mbunge wa Ulanga Mashariki, Celina Kombani ambaye pia ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) kwamba
amekuwa akifanya kampeni za kuwashawishi wataalamu wa wilaya na mkoa
huku akiwataka wananchi kukubali tarafa ya Lupiro ihamishiwe Ulanga
Mashariki kwa maslahi yake binafsi.
Walidai kiongozi huyo huwaeleza watu wa Malinyi kuwa iwapo Lupiro
itaaondoka katika jimbo hilo, makao makuu yatakuwa ni Malinyi, na vivyo
hivyo akiwaeleza wananchi wa Mtimbira kuwa wakifikia maamuzi hayo, basi
makao makuu ya wilaya yatakuwa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa wananchi hao, hofu yao ilizidi zaidi baada ya ziara ya
karibuni wilayani humo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Tamisemi), Hawa Ghasia aliyewaeleza kuwa bado ni ndoto kwa Ulanga
kugawanywa iwapo kutaendelea kuwepo masharti yanayokinzana na taratibu,
kanuni na sheria za upatikanaji wa wilaya mpya.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment