Home » » WAKATI TUNGI WAHOFIA MAGONJWA YA MLIPUKO

WAKATI TUNGI WAHOFIA MAGONJWA YA MLIPUKO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
WAKAZI wa Kata ya Tungi, Manispaa ya Morogoro, wamekumbwa na hofu ya kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (Moruwasa) kutowapatia majisafi na salama kwa muda mrefu.
Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti, Zamu Chande na Stela Fredy, walisema mbali na Moruwasa kufahamu kutotoa huduma katika eneo hilo kwa muda mrefu, imekuwa ikidai kulipwa ankara za maji na kutishia watu kuwaburuza mahakamani.
“Usione hivi, tunatumia maji yasiyo salama kutoka kwenye vidimbwi au maji yaliyotuama baada ya mvua za masika kukatika,” alisema Stella.
Pia alisema mamlaka hiyo imewafanya kitega uchumi chao kwa kuwalazimisha kulipia ankara wasizizotumia huku wakitishiwa kushitakiwa kwa wanaokaidi.
Diwani wa kata hiyo, Deogratius Mzeru, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo.
“Pale ofisini nimefika mara kadhaa, majibu ambayo nimekuwa nikipewea ni kuwa huo ni wajibu na jukumu la mwananchi kuchangia fedha kupata huduma hiyo,” alisema Mzeru.
Mkurugenzi wa Moruwasa hakupatikana kuzinguzia suala hilo kutokana na kuwa kwenye mapuniziko ya mwishoni mwa wiki.
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa