Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgogoro
wa ardhi kati ya Benki ya National Microfinance (NMB) na familia ya
marehemu Ally Rajabu Fuku, anayedaiwa kuwa mmiliki halali wa kiwanja
kinachogombaniwa mjini Morogoro, uliosababisha benki hiyo kushtakiwa
mahakamani, umeibua utata.
Utata huo umejitokeza baada ya baadhi ya nyaraka zilizowasilishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi, kuonyesha kuwa Ally aliwahi kuiandikia Manispaa ya Morogoro barua kulalamikia ujenzi uliofanywa na NMB katika kiwanja hicho kwa madai kwamba, anatambua kuwa bado ni haki yake.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kabla ya kuiandikia manispaa, Ally ambaye anadaiwa kuwa alikuwa akilipia kiwanja hicho kodi ya ardhi, aliwasilisha malalamiko kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, akidai kuporwa kiwanja chake, kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa nyaraka hizo, Desemba 25, 2005, manispaa iliiandikia NMB barua kumbukumbu namba MG/C/41/149 ikiieleza kwamba, imechunguza na kubaini kuwa hakuna milki yoyote iliyotolewa kwa benki hiyo inayohalalisha ujenzi wa benki uliofanyika katika kiwanja hicho.
“Hali hiyo imefanya kwa upande mwingine kuyaona madai ya Ndugu Ally Rajabu kuwa ya msingi,” ilieleza sehemu ya barua hiyo ya manispaa iliyosainiwa na K.M.Kiwera kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa.
Kutokana na hali hiyo, manispaa iliitaka NMB kufuta haki zote zilizokutwa kwenye kiwanja hicho namba 41 Kitalu ‘C’, kilichopo Mtaa wa Uhuru, Manispaa ya Morogoro na iwalipe wahusika fidia ya kiwanja, usumbufu na mali zozote zilizokutwa kabla ya kiwanja hicho kutolewa kwake, kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo, NMB wanadaiwa kupuuza agizo hilo la manispaa na kuendelea na shughuli zao katika eneo hilo.Kitendo hicho kiliifanya familia ya marehemu Ally, ambao ni warithi, ikiwakilishwa na ndugu yao, Omari kufungua kesi namba 15/2008 Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, kudai kurejeshewa eneo hilo na kulipwa fidia ya Sh. milioni 400.
Kesi hiyo ilisikilizwa na kuamuliwa na Jaji Nchimbi, ambaye katika uamuzi wake, aliitambua NMB kama mvamizi. Hata hivyo, mwaka 2010, NMB ilifungua kesi mpya katika Mahakama ya Wilaya ya Morogoro, wakipinga Omari kuwa msimamizi halali wa mirathi ya marehemu Ally.
Kesi hiyo ilisikilizwa na Hakimu Leon, ambaye katika uamuzi wake alisema Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Morogoro, Ponela aliyemthibitisha Omari kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Ally, alikiuka sheria na hivyo, kuharibu taratibu za usimamizi wa mirathi.
Familia ya marehemu Ally haikuridhishwa na uamuzi wa Hakimu Leon, hivyo, ikakata rufaa namba 70/2011 Mahakama Kuu kupinga.
Kesi hiyo ilisikilizwa na Jaji Aboud, iliisha Desemba 15, 2012, lakini uamuzi wake haujulikani unaeleza nini kutokana na jaji huyo, ambaye kwa sasa amehamishiwa Mahakama ya Kazi, kutoutoa hadi sasa.
Katika mgogoro huo, NMB inatuhumiwa kuvamia na kujenga jengo linalotumika kuendesha ofisi za shughuli za tawi lake la Wami mjini Morogoro, katika kiwanja hicho, ambacho inadaiwa kuwa siyo milki yake.
Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa Ally, ambaye alifariki dunia Desemba 26, 2006, anadaiwa kumilikishwa kiwanja hicho na serikali kwa miaka 99 chini ya hatimilki namba 18122, iliyotolewa na Wizara ya Ardhi Julai 29, 1969.
Hata hivyo, nyaraka hizo zinaonyesha kuwa NMB ilivamia kiwanja hicho na kukamilisha ujenzi wa jengo hilo mwaka 1977 kabla ya kuhamia mwaka 1998 na kukitumia kuendesha shughuli za ofisi za tawi lake la Wami mpaka sasa.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment