Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Si hivyo tu, matumizi ya shampoo, hasa zile zinazotokana na mimea,
husaidia katika kuziepusha nywele kutokana na maradhi mbalimbali kama
vile m’ba na mengine yanayosababishwa na bakteria
Matumizi ya bidhaa mbalimbali yamekuwa yakifanyika kutokana na
mazoea tu. Wakati mwingine imekuwa ni vigumu kwa mtumiaji husika
kueleza, umuhimu au faida za bidhaa anayoitumia.
Vivyo hivyo kwa shampoo. Shampoo ni miongoni mwa
vipodozi ambavyo vimekuwa vikitumiwa mara kwa mara, hususan na wanawake.
Aina hii ya kipodozi hutofautishwa kutokana na viungo vinavyotumika
katika utengenezaji wake.
Tofauti hizo zimekuwa zikisababisha kuwepo kwa
viwango tofauti vya ubora kulingana na matakwa ya mtumiaji. Lakini kwa
ujumla wake shampoo ina umuhimu mkubwa katika nywele. Ukiachilia mbali
usafishaji wa nywele shampoo ni muhimu katika kuboresha afya ya ngozi ya
kichwa. Pia hurahisisha ukuaji wa nywele na hivyo kuzifanya ziwe zenye
na rutuba.
Kazi nyingine ya shampoo ni uondoaji wa seli
zilizokufa katika ngozi ya kichwa, jambo linalochangia kutoka nafasi kwa
tundu za hewa katika ngozi ya kichwa kupumua vyema, kitendo
kinachochochea kuota haraka kwa nywele.
Si hivyo tu, matumizi ya shampoo, hasa zile
zinazotokana na mimea, husaidia katika kuziepusha nywele kutokana na
maradhi mbalimbali kama vile m’ba na mengine yanayosababishwa na
bakteria.
Pamoja na kuwa wengi wetu hupendelea kutumia
shampoo, kwa kupenda harufu. Kwa mujibu wa wataalamu, matumizi ya aina
hiyo ni huhatarisha uhai wa ngozi ya kichwa na nywele kwa jumla. Hii
inatokana na baadhi ya kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa
shampoo hususan zile za viwandani kuwa si salama. Kwani badala ya
kurutubisha nywele kutoka na ukali wake husababisha nywele zikatike.
Matumizi ya shampoo zinazotengenezwa na asali,
shubiri, mayai ni sahihi zaidi, kwani husaidia kwa kiasi kikubwa siyo tu
kukuza nywele, bali kuziboresha na hivyo kuziondolea matatizo
mbalimbali likiwamo la kukatika.
Ili kufanikiwa katika yote haya, unashauriwa
kutotumia shampoo kwa mazoea na badala yake kuangalia viungo
vilivyotumika katika utengenezaji .
0 comments:
Post a Comment