Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TIMU 23 za soka kutoka kata za Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro
zimepatiwa vifaa vya michezo kuelekea michuano ya kuibua vipaji ambapo
mechi zake zitakuwa zikifuatiliwa kwa karibu na makocha wa timu za
Yanga, Azam, Simba na Mtibwa Sugar.
Michuano hiyo inayofahamika kama Makalla Cup, itaanzia ngazi ya kata
ikishirikisha timu za vijiji vyote kisha kuchezwa ngazi ya tarafa na
wilaya huku makocha wa timu hizo kubwa wakiangalia vijana wenye vibaji.
Naibu Waziri wa Wizara ya Maji, Amos Makalla, ambaye ni mbunge wa
Mvomero, akitoa vifaa hivyo, alisema michuano hiyo itaanza leo kwa
mfumo wa mtoano huku zawadi ikiwa ni kwa timu ya kwanza na pili.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha
Dakawa wakati wa kugawa jezi na mipira kwa kila kata, Makalla alisema
michuano hiyo imeboreshwa zaidi ikiewemo waamuzi kutoka nje ya wilaya
hiyo.
“Kila hatua ya mashindano ngazi ya kata washindi wa kwanza hadi wa
tatu watapata zawadi, ni pamoja na ngazi ya tarafa hadi wilaya na
zawadi nono zaidi inayofiki sh milioni moja atapewa bingwa wa wilaya ”
alisema Makalla baada ya kugawa vifaa.
Mbali ya kuanika zawadi, alisema katika hatua ya timu nane bora,
atawaleta makocha wasaidizi wa timu za Simba, Yanga, Azam na Mtibwa
Sugar kuangalia vipaji.
Licha ya kutoa mipira kwa ajili ya mashindano hayo, pia alizikabidhi
mipira na jezi timu za soka za vijiji, shule za msingi na sekondari
katika vijiji vya Dakawa, Mlali, Kipera, Mkindo, Kibogoji, Lungo,
Dihinda, Pemba na timu za netiboli ili kuendeleza na kuinua michezo
vijijini.
Baadhi ya timu za soka za Dakawa zilizokabidhiwa jezi na mipira, ni
Small Boys, Young Boys, Veteran FC, Juvinali FC na Dakawa Rangers.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa timu hizo walimpongeza
Makalla kwa kujali maendeleo ya soka na vijana kwa ujumla.
Mbunge huyo ameahidi kuvisaidia pia vikundi vya sanaa vilivyoanzishwa
vijijini vikiwemo vya kareti vya vijiji vya Dihinda na Dakawa
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment