Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Warembo 14 wanaowania taji la Kanda ya Mashariki (Redd’s Miss
Eastern Zone 2014) watashindania taji la vipaji (Talent Award),
lililopangwa kufanyika siku ya Idd Pili kwenye Ukumbi wa Maisha Plus,
Kibaha, Pwani.
Mratibu wa mashindano hayo, Alex Nikitas alisema
kutokana na mashindano hayo ya vipaji, kambi ya warembo iliyopangwa
kuanza Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge, sasa itaanza
Julai 28 kwenye hotel ya Precision mkoani Pwani.
Nikitas alisema maandalizi ya mashindano hayo
yamekamilika na warembo hao, mbali ya kushindana katika vipaji, pia
watatoa msaada kwa kituo cha watoto yatima cha Mkoa wa Pwani na baadaye
kurejea mkoani Morogoro tayari kwa mashindano yaliyopangwa kufanyika
Nashera Hotel Agosti 8.
“Maandalizi yanaendelea vizuri ambapo tunategemea
taji hili msimu huu litakwenda kwa mrembo mwenye vigezo
atakayeiwakilisha kanda yetu vema katika fainali za taifa baadaye mwaka
huu,” alisema Nikitas.
Alisema mashindano hayo yatashirikisha jumla ya
warembo 14 kutoka mikoa minne, ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na wenyeji
Morogoro.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment