Home » » MTIBWA SUGAR YAKATAA KUSAJILI 'MAPROO'

MTIBWA SUGAR YAKATAA KUSAJILI 'MAPROO'

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Wakati timu nyingine zikijizatiti kuimarisha vikosi vyao kwa kufanya usajili nje ya nchi, imekuwa tofauti kwa kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime, ameweka wazi kuwa hana mpango na wachezaji wa nje ya Tanzania.
Kocha huyo amebainisha kuwa hana mpango na wachezaji wa nje na badala yake atawatumia wazawa ambao anaamini wana viwango zaidi ya wale wanaotoka nje ya nchi.
“Sioni sababu ya kusajili mchezaji kutoka nje na kumlipa fedha nyingi wakati wachezaji wazawa wapo na wana uwezo,” alisema Mexime na kuongeza kuwa kikosi chake kitaingia kambini Jumapili hii Manungu kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayoanza mwishoni mwa mwezi ujao.
Wakati huo huo, kikosi cha Mbeya City kimepanga kuanza kambi Julai 15 kujiandaa na ligi, katika kambi iliyopangwa kuwekwa jijini Mbeya
 Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa