Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUNDI la hamasa na ushangiliaji la Klabu ya Simba tawi la Nguvu
Moja la jijini Dar es Salaam, wamefiwa na shabiki Mawazo Ramadhani
‘Kidedea’ aliyefariki dunia usiku wa kuamkia Julai 5, baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Mwili wa Kidedea ulisafirishwa hadi mjini hapa na kuzikwa jana katika
makaburi ya Kola na kuvuta mamia ya watu wakiwemo wapenzi wa Simba na
Yanga.
Kabla na baada ya mazishi, kwa nyakati tofauti baadhi ya mashabiki
walisema Kidedea alikuwa ni mdau wa kweli wa Simba akiwa mwanachama
tangu Julai 21, 2011.
Kwa upande wake, Salim Simba wa tawi la Vuvuzela na Shamte Mkumba
tawi la Yanga Boma, walielezea kuwa kifo cha Kidedea ni pigo kwa Simba.
Walisema mwili wa Kidedea ulisafirishwa hadi Morogoro kutekeleza kauli yake ya kutaka kuzikwa kwao.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment