Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANANCHI wa Mkoa wa Morogoro wametakiwa kujitokeza kwa wingi
kuchangia damu kwa hiari katika maadhimisho ya Wiki ya Damu, ikiwa ni
utekelezaji wa mpango wa taifa wa damu salama.
Wito huo ulitolewa na Ofisa uhamasishaji elimu kwa umma, Wille
Mathew, katika kituo kidogo cha uchangiaji damu na kusema kuwa zoezi
hilo linatarajiwa kuanza rasmi Machi 18, mwaka huu na kudumu kwa muda
wa wiki moja.
Alisema zoezi hilo litashirikisha vyuo vilivyopo mkoani humo kikiwemo
chuo cha ujenzi, Jordan University, chuo cha mifugo, Chuo cha Uislamu,
Saint Joseph pamoja na taasisi nyingine za elimu zikiwemo Lutheran
Junior Seminary na Shule ya Sekondari Presybeterian.
Chanzo:Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment