Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bao lililofungwa na James Mganda dakika ya 26 lilitosha
kuiwezesha Polisi Morogoro kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Maji Maji ya Songea
katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa
Jamhuri Morogoro.
Polisi Moro inayonolewa na kocha Richard Adolph
ilikuwa ikihitaji ushindi wa namna yoyote katika mechi hiyo, ambapo
dakika ya sita nahodha wake Nahoda Bakari alimimina krosi iliyomkutana
na Mfuko Abdallah ambaye aliukwamisha mpira nyavuni.
Bao hilo liliwachanganya Majimaji na kusababisha
mambo yawaendee kombo kwani dakika ya 26 waliruhusu kufungwa bao la pili
na, James Mganda anayechezea timu ya taifa ya vijana (Serengeti Boys
U17).
Mganda alifunga bao hilo baada ya kutumia vema pasi nzuri ya Nicolaus Kabipe.
Kipindi cha pili Majimaji inayonolewa na kocha
Hassan Banyai ilikianza kwa nguvu, ambapo ilipata bao la kufutia machozi
dakika ya 79 lililofungwa na Anthony Mwingira.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment