Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
UANDIKISHAJI wa watoto wenye ulemavu katika shule za msingi
wilayani Kilombero umeongezeka kutoka watoto 131 mwaka 2012 hadi watoto
160 mwaka jana.
Hayo yamo kwenye taarifa ya utafiti wa pili juu ya vikwazo
wanavyopata wenye ulemavu katika kupata elimu uliofanywa na vyama
vitano vya wenye ulemavu wilayani Kilombero kupitia mradi wa kuboresha
uelewa na utetezi kwa jamii (ICAAD) na taasisi ya Kesho Trust Tanzania
kwa kufadhiliwa na shirika la misaada ya kimaendeleo nchini Uingereza
(UK Aid).
Mratibu wa mradi wa ICAAD Kilombero, Lucas Liombechi, alisema vyama
vilivyoshiriki katika utafiti huo Kata ya Ifakara, Kibaoni na Lumemo ni
Chama cha Wasioona (TLB), Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA), Chama
cha Walemavu Tanzania (Chawata), Chama cha Albino Tanzania (TAS) na
Chama cha Wenye Ulemavu Tanzania (TAMH).
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment