Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Maofisa
wanyamapori mjini Ifakara mkoani Morogoro wamekamata vipande 14 vya
meno ya tembo pamoja na meno mengine mazima manne yote yakiwa na
thamani ya Shilingi milioni 120.
Katika kamata hiyo, mtuhumiwa Sudi Nyumbi mfanyabashara wa jijini Dar es Salaam, alinaswa akiwa katika kijiji cha Katindiuka wilayani Kilombero akiwa na vipande 14 vya meno hayo yenye thamani ya Sh. 72,000,000 na manne yenye thamani ya sh 48,000,000.
Akizungumza na NIPASHE wakati wa mahojiano, Afisa wa Wanyamapori Kilombeo, Madaraka Amani alisema mtuhumiwa alinaswa Jumanne wiki hii wakati huo akitoka ndani ya lango la kizuizi cha ukaguzi la Kidatu akielekea Dar es Salaam.
Amani alisema askari wa wanyapori waliokuwa kwenye doria kijiji cha Katindiuka waliwaona watu wawili wakiwa kwenye baiskeli na walipokuwa wakiwafuatilia walikimbia na kuitelekeza baiskeli pamoja na meno hayo manne.
Hata hivyo, alisema meno hayo manne inaonyesha kuwa yalikuwa yamechimbiwa ardhini na kwamba walikwenda kuyafukua. Aliongeza kuwa kabla ya oparesheni tokomeza ujangili ulikuwa umeshika kasi lakini baada ya kusimamishwa unaanza tena.
Ofisa tarafa mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema wanafanya juhudi za kupambana na ujangili ila tatizo lililopo ni kukosekana kwa ushirikiano kesi zinapokuwa mahakamani.

SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment