Home » » Maambukizi ya VVU yazidi kupungua nchini

Maambukizi ya VVU yazidi kupungua nchini

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Dk. Fatuma Mrisho.
Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) yanazidi kupungua mwaka hadi mwaka nchini.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids),  Dk. Fatuma Mrisho wakati akifungua semina kwa mahakimu, maofisa wa polisi na wanasheria wa Serikali wa   mikoa ya Dae es Salaam, Pwani na Morogoro

Dk. Mrisho alisema takwimu zinaonyesha kuwa maambukuzi ya ukimwi yamepungua kwa kiasi kikubwa nchini.

Alisema takwimu zinaonyesha kuwa   kuwa Tanzania Bara na Visiwani  kuanzia mwaka 2003 hadi 2004 maambukizi hayo yalikuwa ni asilimia 7.

Mwaka 2007 hadi 2008 yalishuka mpaka kufikia asilimia 5.7 na mwaka 2011 hadi 2012 yalishuka   zaidi hadi  kufikia asilimia 5.1 kwa kiwango cha kitaifa.

Tanzani Bara pekee kiwango cha maambukizi ya VVU  ni asilimia 5.3 zaidi ya kiwango cha kitaifa.

"Kila mtu kwa namna moja au nyingine anaguswa na ukimwi maana hakuna ukoo, kijiji, wilaya na mkoa usio na mtu anayeishi na VVU na hivyo hadi nchi nzima inaguswa na hali hiyo, " alisema Dk.. Mrisho.

Aliwaasa washiriki hao wa semina na Watanzania kuacha  ngono zembe   ili maambukizi ya ukimwi yaweze kupungua na kufikia kiwango cha asilimia sifuri hadi kufikia mwaka 2015.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa