Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAHANGA wa mafuriko katika maeneo ya Dumila, mkoani Morogoro
wanakabiliwa na hali ngumu ya ukosefu wa makazi baada ya nyumba zao za
muda (mahema) kuezuliwa na kimbunga kilichoambatana na mvua.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili kwa njia ya simu,
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mateteni Dumila, Iddi Mangilile, alisema
mvua hizo zimechangia kuharibika kwa mahema hayo.
Mangilile alisema mvua ilianza kunyesha nyakati za mchana na
kusababisha ukosefu wa makazi huku familia nyingi zikiishi kwa
kutangatanga.
Alisema licha ya Chama cha Msalaba Mwekundu kukarabati mahema hayo
bado wapo katika hali ngumu kwani familia nyingi zimeshindwa kuendelea
kujishughulisha kama ilivyokuwa awali.
“Tunashukuru sana Chama cha Msalaba Mwekundu kuwa nasi bega kwa
bega kipindi chote cha matatizo ya mafuriko hadi sasa kwani mvua bado
zinaendelea kunyesha na zinaambatana na upepo mkali, hivyo bado tupo
katika wakati mgumu,” alisema.
Naye Rais wa chama hicho, Dk. George Nangale, alisema
wanashirikiana na serikali ili kuwapatia familia 400 maeneo ya kuishi
ya muda kwa lengo la kujihifadhi katika kipindi hiki.
Alisema waliwapatia makazi hayo ya muda wakazi wa vijiji hivyo
ambayo yalijengwa kwa ustadi lakini mvua iliyoambatana na upepo
iliyonyesha juzi ilichangia kuezuliwa kwa nyumba hizo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment