Kukosekana kwa elimu ya ufuatiliaji fedha za umma kwa wananchi
wengi, kumesababisha ongezeko la utekelezaji miradi ya maendeleo hususan
maeneo ya vijijini kufanywa chini ya kiwango.
Baadhi ya wananchi wa Mji Mdogo wa Kimamba,
wilayani Kilosa; Ramadhan Liwest, Aishi Ally na Yahya Mhina walisema
hayo walipozungumza na waandishi wa habari.
Walishauri ni vyema jamii ikapewa mafunzo ya
kuwajengea ufahamu wa kuhoji mapato na matumizi, hasa idara zinazogusa
moja kwa moja jamii; Elimu na afya.
Kauli ya wananchi hao imekuja huku tayari asasi
isiyokuwa ya Serikali ya Kilosa African Youth Organization (Kayo), ikiwa
imeanza kuwezesha wananchi hao kuhusu mbinu za Ufuatiliaji Matumizi ya
Rasilimali za Umma (Pets) kwenye idara ya afya.
Mratibu wa Kayo, Ramadhan Nassoro na Katibu wake,
Juma Mseti kwa nyakati tofauti walisema wameamua kutoa mafunzo hayo ili
wananchi wajitambue na kufahamu wajibu wao kufuatilia fedha na
rasilimali za umma.
Nassoro alisema wananchi wanaweza kufanya jukumu
hilo kama vikundi kwa kufuatilia matumizi na mapato, ikiwamo vituo vya
afya na zahanati na kwamba kufanya hivyo kutasaidia ufanisi wa
utekelezaji majukumu mbalimbali.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment