Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (Sua) kwa kushirikiana
na vyuo sita kutoka nchi za Kenya, Uganda, Zambia na Norway zimeanzisha
mradi maalumu wa kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo wataalamu wanaofanya
utafiti kuhusiana na Afya ya Mazingira na Viumbe vya Majini (Trahesa).
Hayo yalibainishwa mkoani hapa katika mkutano na wadau mbalimbali wa
sekta ya uvuvi nchini na Mkuu wa mradi huo, Profesa Robinson Mdegela.
Alisema mradi huo utasaidia kuimarisha uwezo wa matumizi sahihi na
endelevu sekta ya uvuvi.
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment