Home »
» Polisi yatoa onyo kwa wafanyabiashara Moro
Polisi yatoa onyo kwa wafanyabiashara Moro
Jeshi
la Polisi mkoani Morogoro limewataka wafanyabiashara wenye mashine za
EFD wanaolazimishwa kufunga maduka yao na kikundi cha wafanyabiashara
wachache wasio na mashine hizo kutoa taarifa ili sheria ifuate mkondo
wake.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Morogoro, Faustin Shilogile, kufuatia baadhi ya wafanyabiashara
kulalamika kuwa kuna kundi la wahuni linalotumiwa na baadhi ya
wafanyabiashara kuwashinikiza wengine kufanya mgomo ili kupinga mashine
hizo.
Alisema mfanyabiashara akifunga duka lake kwa matakwa yake
mwenyewe si kosa, lakini asilazimishe wengine kufunga maduka, kwani
kufanya hivyo ni kutenda kosa.
"Jeshi la Polisi linafanya doria
katika kila mtaa ili kukichunguza kikundi hicho kinachozuia
wafanyabiashara wengine kufungua maduka," alisema Shilogile.
Alisema
kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa ajili ya ulinzi wa raia na mali zao ikiwa
pamoja na kusimamia sheria za nchi zilizowekwa kwa mujibu wa katiba ya
nchi, hivyo hakuna sababu ya kunyamazia matukio yeyote yenye nia ya
kuvunja sheria zilizotungwa kwa mujibu wa sheria ya nchi," alisema.
Jana
wafanyabiashara wa manispaa ya Morogoro walifunga maeneo yao ya
biashara zao kwa lengo la kugomea matumizi ya mashine za kielektroniki
za EFD
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment