Morogoro. Jumuiya wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama
cha Mapinduzi(CCM) Wilaya ya Mvomero, imelaani vikali kauli zilizotolewa
na Mkuu wa Wilaya hiyo, Antony Mtaka kwa kuwafananisha wanawake na
‘kondomu’ ama tambara la deki.
Baadhi ya wanawake ambao ni Wajumbe wa Baraza la
UWT Mvomero ambao hawakutaka majina yao kuandikwa gazetini walisema mkuu
huyo wa wilaya aliwataka wanawake kutokutumiwa vibaya wakati wa chaguzi
zijazo kauli ambayo wanawake hao hawakupendezwa nayo.
Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro
wanawake hao walisema baada ya kufanyika kwa baraza Desemba 12 mwaka
huu katika ofisi za CCM Dakawa wilayani Mvomero ambapo DC Mtaka alikuwa
mgeni rasmi, wamekaa na kutafakari kauli hiyo na kuona kuwa ni ya
udhalilishaji kwa wanawake kufananishwa na kondomu au tambara la deki
Walidai kuwa mkuu huyo wa wilaya alialikwa kwenye
baraza hilo na baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na wajumbe
aliwaambia wasikubali kutumika kama kondomu ama tambara la deki na
wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi ujao.
“Kauli alizotoa Mtaka si nzuri zimetusikitisha
sana, anatuambia sisi kinamama ni kama kondomu ambayo ikishatumika
inatupwa, ama tambara la deki ukidekia halina thamani tena, kauli hii si
ya kiungwana walisema.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka akijibu
tuhuma hizo, alikiri kutumia kauli hizo na kwamba hakuwa na nia mbaya
kama wao walivyofikiria isipokuwa hizo ni siasa chafu za baadhi ya
wanasiaa wa Mvomero .
Mtaka alisema Jumuiya hiyo ni kubwa ndani ya CCM
na kwamba kuna viongozi wengi wa siasa lakini cha kushangaza hakuna hata
mmoja aliyeichangia jumuiya hiyo ili iweze kufanikiwa.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment